0 0
Read Time:34 Second

Kwa mara ya kwanza leo Rais wa Jamhuri ya Muungano ameongea na Taifa kupitia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tutakamilisha madaraja
makubwa
-Rais Samia Suluhu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema watatekeleza miradi yote ya kimkakati ikiwemo ukamilishaji wa madaraja makubwa yanayoendelea kujengwa nchini.

Rais Samia amesema maeneo ya kimkakati ambayo Serikali itahakikisha inayakamilisha ni pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa yakiwemo ya Kigongo-Busisi, Wami, daraja la Tanzanite na daraja la Pangani.

Madaraja yote hayo yanayojengwa yanasimamiwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Mheshimiwa Rais amesema Serikali tayari imekamilisha miradi ya ujenzi wa barabara wa kilomita 3,537 na madaraja makubwa 12 nchini kote.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %