0 0
Read Time:2 Minute, 56 Second

George Michael Uledi.
Kyela,
Mbeya.
May 13, 2021.

Naona kuna umuhimu sasa sera yetu ya uwekezaji kuwa na mtazamo mpana kwa kuainisha mambo ya msingi kuhusu uwekezaji gani ambao Tanzania kama Nchi ingependa kuuona ukifanyika hapa Nchini.

Katika kutekeleza dhana ya uwekezaji makini”responsible investment” tunapaswa kuangalia mambo fulani fulani ya msingi kwa Taifa kwa ajili ya kulinda maslahi yetu kama Nchi na kama Taifa!

Sera yetu ya Taifa ya uwekezaji lazima itaje maeneo ya kimkakati ya uwekezaji ambayo yanaweza kuleta tija kwa Taifa lakini bila kuathiri usalama wetu na kuwa na mpango wa kitaifa ya jinsi gani tunaweza kuwatumia matajiri wetu kuwekeza mitaji yao ndani ya Tanzania katika mfumo wa kuunganisha mitaji yao kwa pamoja!

JE NI MAENEO GANI TUNATAKA WAWEKEZAJI WAJE KUTUSAIDIA?

1.Lazima kama Taifa tuainishe maeneo mkakati ambayo wawekezaji kutoka nje wangeweza kuja kuwekeza kwa sababu ni wazi kuwa hatuwezi kukaribisha wawekezaji wa nje katika kila eneo.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kulinda maslahi ya Taifa kwani sio salama sana kwa Taifa Uchumi wake wote kuendeshwa na wageni “Kilimo,viwanda,Madini,utalii na mengineyo.

2.Lazima tuandae watu wetu pia washiriki katika kuwekeza katika sekta nyeti mfano madini kwa kuhakikisha tunakuwa na kampeni maalum ya kuwashawishi kuwekeza kwa kuunganisha mitaji yao!Tunashindwaje kuwashawishi watu kama Salim Bhakresa na Mohamed Dewji kuwekeza katika sekta za madini?

Ni hatari sana robo tatu ya shughuli za shughuli za uchumi wa Nchi kuendeshwa na wageni kwani Wafanyabiashara wa kigeni kwa maana ya wawekezaji wanaweza kuiweka Serikali mfukoni na Serikali kukosa sauti dhidi yao!

3.Lazima tuanze kufikilia kuwa na balansi kati ya kuwa na wawekezaji wazalendo na wawekezaji kutoka nje kwani huo ndio usalama wetu kama Nchi lasivyo tutakuwa tunafanya kosa kubwa katika kuyalinda maslahi yetu kama Taifa.

Serikali lazima kuanza kufikilia hilo na kuhakikisha kuwa katika kutekeleza dhana hii ya uwekezaji lazima twende mbali kwa kuwawezesha Wazalendo na Watanzania kuwekeza.Tutakuwa Nchi ya ajabu kama tutaenda kuweka rehani Uchumi wetu wote na kuwakabidhi wageni huku tukibaki kukusanya kodi tu!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %