
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 13,2021.

Ni wazi kuwa Nchi ya Tanzania inaweza ikachelewa kwenda kwenye Uchumi wa juu kwa sababu kubwa moja ambayo ni kukosa kujiamini kama Nchi katika utekelezaji wa mambo yake hasa miradi ya kimkakati!Mradi wa uchumi wa gesi iliyosindikwa kwa maana ya “Liguefied Natural Gas” ambao unatarajiwa kutekelezwa katika Mkoa wa Lindi,pekee yake unaweza kuipa
Tanzania mapato ya shilingi 10 Trilioni kwa mwaka kwa bei ya soko la dunia la sasa.
Lakini tatizo la Nchi ya Tanzania ni moja tu nalo lipo katika kuamini kuwa hakuna mradi mkubwa wanaweza kuutekeleza bila watu kutoka nje ya Tanzania kwa maana ya uwekezaji wa kutoka Nje na hapo ndio Tanzania kama Nchi inaendelea kukwama,
miaka nenda rudi.
Tanzania ingekuwa na uthubutu wa angalau wa asilimia 50 tu katika kutekeleza miradi yake ya kimkakati kwa kutumia watu wake na mashirika yake ya ndani ingeweza kuwa Nchi yenye uchumi mkubwa barani Afrika ndani ya miaka michache ijayo!
Rasilimali gesi pekee yake inaweza kuifanya Tanzania kuwa tajiri ndani ya miaka kumi tu achana na vitaru vya mafuta yaliyopo ndani ya ukanda wa bahari ya Hindi!Utajiri wa madini ya kila aina yaliyojaa ndani ya ardhi ya Tanzania ungeweza kuifanya Tanzania kuwa tajiri kuliko Nchi yoyote katika ukanda wa SADC na Afrika Mashariki lakini Tanzania inakwama kwa kukosa Kiongozi jeuri mwenye maono ya ‘yes we can’!
WAPI TANZANIA TUNAKWAMA KATIKA KUTEKELEZA MIRADI INAYOBEBA UTAJIRI MKUBWA MPAKA TUKAHITAJI WAWEKEZAJI TOKA NJE?
Hivi ninavyoandika Shirika la Taifa la mafuta la Qatar yaani Qatar Petroleum kwa hapa kwetu tunaweza kuliita TPDC lipo kwenye Mpango kabambe wa kutanua uzalishaji na usindikaji wa gesi asilia yaani LNG kwa kuwekeza fedha ya Serikali kwa asilimia 50 mpaka kufikia uzalishaji wa tani za gesi asilia 126 kwa ajili ya kuuza nje ya Nchi ya Qatar, Waziri wa Nishati wa Qatar Mh Saad Al – Kaabi anasema,
“..Qatar aims to be the World’s biggest producer of Liguefied Natural gas for at least the next two decades,capitalising demand as the World transition from Oil and Coal to Cleaner energy”LNG economy”.
1.Sasa najiuliza TPDC anashindwaje kufanya haya mpaka tumeamua kuwaita Shell ya Wadachi?Je tumeshindwa kuwaita Shell kwa kuwakodi kuja kutujengea mradi tu na kutuachia biashara ya gesi ya kusindika asilia tuendeshe wenyewe?
2.Kama kila siku tunachukua mikopo kwani hatuwezi kuchukua mikopo huko duniani na kuwekeza katika sekta ya kusindika gesi asilia mpaka tuanze kutafuta ubia kutoka nje?Tunakwama wapi kwa kuamua kutapanya utajiri wetu?,kwanini Nchi kama Qatar haya mambo hayapo?Kwanini mambo haya yanatokea Afrika tu?
- Kama Taifa tumeweza kuthubutu kuanzisha ujenzi wa SGR,bwala la umeme,ununuzi wa Ndege kwani tungeshindwa kuwekeza katika usindikaji wa gesi asilia?!Kwanini Kampuni ya Shell isije hapa kama”Project Contractor” tu na sio mbia au mwekezaji?Yaani mpaka leo tunashindwa kuwekeza katika miradi mkakati ambayo ingetupa faida kwa muda mrefu lakini faida yote ingebaki hapa Nchini.
4.Utawala wa Serikali ya awamu ya tano ulisitisha mazungumzo na Wawekezaji hawa kwa maana ya Shell ya Udachi na Equinor ya Norway mwaka 2019 kwa lengo la kupitia upya mkataba wa uzalishaji na mgawanyo wa mapato yaani “PSA”.
- Nenda kokote duniani iwe ya uchina,Marekani,Uwingereza na Ufaransa ambao wanaangaika kuja kuwekeza Afrika kama leo wanaweza kukupa gesi yao au madini yao yoyote kwa kigezo cha Uwekezaji wa Nje!Labda watakwambia wekeza katika Kilimo ambacho kwao sio Ishu kubwa lakini sio wakupe gesi,coal,copper nani kakwambia?.Haya mambo ya FDI’s kwenye utajiri wa madini ya mafuta na gesi yanatokea Afrika tu!
Kwanini tunakosa kuwa na ndoto kubwa kama Taifa?Tanzania haiwezi kuwa Taifa ambalo linakaribisha wawekezaji katika kila eneo huku tukitegemea kuwa Taifa kubwa!Ni lazima tuchague wapi turuhusu wageni na miradi hipi tufanye wenyewe kwani hauwezi kuwa Taifa kubwa kwa kuruhusu rasilimali zako “critical” kuendeshwa na wageni kwani hakuna kitu kama hicho duniani.
NINI TUFANYE KAMA TAIFA KATIKA KUHAKIKISHA RASILIMALI ZETU ZA KIMKAKATI ZINAVUNWA NA SISI WWNYEWE!








