0 0
Read Time:6 Minute, 8 Second

UJUMBE KWA MABALOZI WETU WAPYA

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 25,2021.

Sikushangaa kuona uteuzi wa maofisa wa juu kutoka jwtz katika listi ya mabalozi wapya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan hivi karibuni!Hii inatoa ishara kuwa Taifa limejipanga kwenda kutekeleza diplomasia yetu ya mambo ya nje kwa kishindo kikubwa.

JICHO LA ULEDI

Diplomasia yetu ya mambo ya Nje kwa sasa kama Taifa ili iweze kutupeleka tunakotaka lazima iwe na uwezo wa kusimamia na kulinda mambo makubwa matatu;

  1. Kwanza ni kuangalia usalama wetu kama Taifa kwa kuangaza maadui wa nje na mipango yote ya nje dhidi ya Tanzania ambayo inaweza kuleta athari za moja kwa moja kwa Taifa letu.

Hakuna mtu mwingine wa kuweza kulinda maslahi ya Usalama ya Tanzania nje ya mipaka yetu zaidi ya Balozi zetu na katika hili hakuna ubishi kuwa maofisa wa juu wa jwtz wanaweza kutekeleza jukumu hili kwa Weledi kuliko mtu yoyote!Sina wasiwasi kuwa Afande Meja Jenerali Makanzo, Mkuu wa kamandi ya jeshi maji anaiweza kazi hii vizuri kabisa.

Sina wasiwasi kabisa na “jasusi”Luteni Jenerali Yakubu Mohamed,Mnadhimu wa jwtz kwamba anaweza kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa kwenda kuziba maeneo ambayo tulionekana tumepwaya kama Taifa ambapo taarifa nyingi za kutuvuruga kama zilikuwa zinatoka nje ya mipaka ya Tanzania

2.Pili,wajibu wa Balozi ni kuyatafuta maslahi yetu ya kiuchumi nje ya mipaka yetu kwa njia tofauti yaani njia za kidiplomasia”economic diplomacy” na wakati mwingine njia za kificho” foreign economic intelligence”.

Tunahitaji watu wa kutupa taarifa sahihi kwa ajili ya kuweza kutekeleza maslahi yetu ya kiuchumi nje ya mipaka yetu kama uwekezaji,mikopo nafuu na mengine mengi ambayo hayapaswi kusema hapa.Mabalozi wetu wanapaswa watuambie sehemu dhaifu kisera na kisheria huko nje ambazo tukizitumia tunaweza kupata faida na maendeleo makubwa kama Taifa.

Mabalozi wetu wana wajibu wa kutuambia kuhusu fursa za kiuchumi tunazoweza kufaidika nazo kutoka katika taasisi za kimataifa za kifedha kama IMF,WB,G8,Paris Club na mashirika mengine lakini pia lazima watuambie hatari za baadhi ya mikopo ambayo tukiichukua kutoka taasisi hizo Kubwa tunaweza kupata madhara fulani fulani”Warning”.

3.Tatu,wajibu wa sasa wa Balozi zetu ni kuhakikisha wanaweza kuitangaza misimamo,maono na dira ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kulinda heshima na Uhuru wetu”Managing Country’s positive image”.Bila kuwaambia wenzetu sisi ni nani kama Taifa,tuna maono gani kama Taifa na dhamira yetu ni nini basi hatuwezi kufanikisha malengo yetu nje ya mipaka.

Wajibu wa mabalozi hawa ni kusimamia kikamilifu “good image” ya Tanzania nje ya mipaka ili kuweza kutufanya kuaminika hivyo kuweza kuvutia mitaji na kujenga mahusiano katika kila nyanja kwa manufaa ya pande mbili.

Kwa sasa naona wazi kuwa mipango yetu ya kuwa Taifa kubwa na Taifa tajiri isingeweza kufanikiwa kwa haraka na kuwa”Sustainable” bila kuwa na listi ya namna hii!Hapa pongezi nyingi ziende kwa Mama Samia na washauri wake wakuu.

Kwa sasa ni wazi kuwa bila kuwa na “a strong economic intelligence unit” zetu ambazo zinawajibika kutuambia ni wapi tunaweza kwenda kama Taifa ambako bado kuna udhaifu wa sera za kiuchumi na udhaifu wa usimamizi wa rasilimali za Taifa “Instability” ambako wafanyabiashara na Serikali tunaweza kupenya na kuvuna utajiri kwa maslahi ya Tanzania,itakuwa ni kazi bure!

Na sisi kama Taifa ni Leo wakati sahihi sasa lazima tuanze kuyatafuta maeneo dhaifu duniani kwa malengo hayo hayo ya kuvuna utajiri wa mataifa mengine kupitia makampuni yetu kama Twiga Corporation,Kampuni zingine za kizalendo pamoja na wafanyabiashara wengine wa kitanzania wawezeshwe kupata mitaji na Serikali ili wakafanye kazi ya kutafuta maslahi zaidi ya Taifa katika mataifa mengine dhaifu.

Uteuzi wa mabalozi ni moja lakini la muhimu ni lazima Serikali yetu iwe nyuma ya mpango huu kwa kuviwezesha vitengo vya “economic intelligence” katika Balozi zetu na katika vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama ili viweze kusaidia Serikali ya awamu ya sita kuweza kupata taarifa sahihi kwa wakati kuhusu fursa za kiuchumi katika mataifa mengine kwani bila kuwa na taarifa za ndani na za uhakika hatuwezi kutekeleza dhana hii kama Taifa na kwenda kutafuta maslahi katika mataifa mengine duniani.

Unapokuwa na makampuni kitaifa na ya kizalendo kama Azam Group katika Nchi jirani au nje ya mipaka kwanza unakuwa na uhakika na mambo makubwa matatu; kwanza kujenga uwezo wa makampuni yako za kizalendo kushindana katika masoko mengine ya nje ya mipaka,pili makampuni haya uweza kuvuna utajiri kutoka Nchi jirani kupitia kuuza bidhaa na huduma lakini la muhimu kabisa,mnaweza kutumia makampuni haya au biashara hizi kutekeleza mipango yenu ya kiulinzi na kiusalama kama Taifa nje ya mipaka yenu.

WENZETU WANAFANYA KWA NGUVU KUBWA NA SISI LAZIMA TUFANYE LAKINI KWA”MODEL” YETU.

Mataifa mengi kwa sasa uunda vikosi maalum kwa ajili ya kutekeleza dhana ya “Foreign economic intelligence”kwa kusoma fursa na udhaifu wa Nchi nyingine na kuzitumia kama daraja la kuvuna utajiri katika mataifa Yao.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %