0 0
Read Time:3 Minute, 0 Second

Na Dr Yahya Msangi

Kwa muda sasa haswa baada ya kifo cha JPM (Allah amrehemu) spika bunge la JMT amekuwa anatoa kauli zenye ukakasi.

Alianza na suala la bandari. Juzi hapa anadai nchi “huko duniani” zinafanya “less governance”. Yaani serikali zinajiweka mbali na raia ili kuwaachia wajinafasi. Akatolea mfano wa korosho. Spika akadai serikali imeingia kwenye korosho kuliko inavyohitajika.

Ukakasi huu unatokana na tabia ya rangi mbili (tetracycline behavior). Huku njano kule nyeusi! Spika huyu aliunga mkono uamuzi wa kutojenga bandari na zoezi la serikali kudhibiti zao la korosho. Leo amesubiri JPM hayupo anapinga!

Tabia hii ya rangi mbili (tetracycline) imewaathiri wengi.

Hakika walio wema ni wale waliosimamia wanachoamini toka JPM akiwa hai na baada ya kuitika wito wa Allah. Walisema wanachoamini. Walichodhani ni vyema na walichohisi ni kosa. Hakuna aliye mkamilifu.

Kwa upande wa pili wapo wanaougua “aspirin behavior”. Aspirin ina rangi moja tu! Wao ama wanaona mabaya tu au wanaona mazuri tu.

Spika ni kama ugonjwa huu pia umemuathiri. Akisimama siku hizi ni kutoa kauli zainazoashiria hakuna jema alilotenda JPM. Ukitafakari kauli za bandari na “too much governance” kwenye korosho hutasita kubaini haya madongo yanamlenga nani!

Lakini ukiacha haya kuna jingine jipya ambalo sina uhakika ndivyo bunge linavyopaswa kuendeshwa au kama hâta kanuni zinaruhusu. Sijaona mawaziri wakihoji au hâta waziri mkuu kuhoji. Sijamsikia Mwanasheria Mkuu akihoji!

Mara kadhaa spika amegeuza nafasi yake kuwa mshauri au hâta kuelekeza mawaziri nini cha kufanya. Tena mara nyingi katika hali ya kudhalilisha mnoo. Hatari yake ni kuwa mipango na bajeti za wizara zinaweza kuamuliwa na kiti cha spika. Mifano: mifugo kuingia hifadhi, masuala ya utalii na mashirika ya umma kama DAFCO, NARCO, etc.

Tatizo linakuwa hili: bungeni masuala huamuliwa baada ya kujadiliwa kwenye ‘floor’. Inapotokea spika anatoa maagizo kwa lugha ya “hebu serikali au wizara mliangalie hili” kwa mawaziri bila kujadiliwa inakuwa sio “procedural”!. Sio tena bunge linashauri au kutoa maagizo kwa wizara au serikali bali mtu mmoja aitwaye Spika.

Najiuliza hivi kwa nini mwanasheria mkuu haoni hili? Wanamuogopa? Hivi hawaoni baadhi ya ushauri wake ni upotoshaji?

Chukulia suala la uvuvi haramu. Spika anadai nyavu zisitaifishwe au kuteketezwa! Si itakuwa balaa wizara ikitekeleza? Spika anajua athari za uvuvi haramu kwa vizazi vijavyo ?

Kuhusu mifugo hifadhini anadai isitaifishwe. Lakini hasemi nini kifanywe? Spika alimkosoa Lissu alipodai ataruhusu mifugo ilishwe mbuga za hifadhi! Léo anatoa hoja ileile bungeni!

Tuchukulie mifugo imeingia shamba la mahindi? Sheria iseme waachiwe kwa kuwa wanaoichunga ni watoto? Serikali ndio imlipe mkulima? Na je kama wanaoichunga ni watu wazima? Wao waadhibiwe Watoto waachiwe? Si itachochea watoto washinde machungani wasiende shule? Nilidhani spinal angekenea tabia ya kuwaacha watoto wachunge tena jirani au ndani ya mbuga zenye wanyama wakali!

Kuhusu kufufua kina NARCO, DAFCO, NAPOCO, etc na wenzao spika anataka wizara iache kwa kigezo kuwa yalikufa. Hivi spika hajui TRC, ATCL na wenzao zilikufa na JPM akazifufua? Nazo zingeachwa kufufuliwa ndio ingekuwa Sawa?

Hivi kama shirika lina tija lisifufuliwe? Ilinishangaza reaction ya Waziri na Naibu wake kutikisa vichwa kuashiria wanakubaliana na Spika! Walipaswa wasimame waeleze umuhimu wa baadhi ya mashirika na namna watakavyo yalinda yasihujumiwe tena. Mfano wakati wa vita na njaa mashirika haya yaliokoa jahazi. Kwa umri wa spika atakuwa aliona!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %