![](https://www.tzabroad.com/wp-content/uploads/2021/05/social-media-danger.png)
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 31,2021
![](https://www.tzabroad.com/wp-content/uploads/2021/05/jicho-la-uledi-4.jpg)
Wataalam wa sekta ya mawasiliano na habari wanajua kuwa vyombo vya habari ni bunduki na maudhui ni kama risasi ambapo yasipoweza kuangaliwa na kuachiwa holela basi vyombo vya habari vinaweza kuleta madhara makubwa katika amani na umoja wa kitaifa hivyo kuchochea vurugu na kutokuheshimiana.
Tukiwa darasani katika vyuo vikuu vyetu mara zote tunafundishwa jinsi ya kuhakikisha tunavitumia vizuri vyombo vya habari ili kuleta mchango chanya kwa Taifa kwani pamoja na vyombo vya habari kuthibitika kuweza kuleta maendeleo chanya kwa Taifa lakini pia imethibitika kuwa vyombo vya habari vikitumika vibaya uweza kuleta vita,kubomoa umoja wa kitaifa na mengine mengi yasiyo mema!Mfano ni Radio Mencoline pale Rwanda!
Wakati huu kuna mjadala mkubwa unaendelea katika sekta ya habari kwamba vyombo vya habari vya mwanzo”traditional media” ni kama nafasi yake imechukuliwa na vyombo vya habari za kisasa yaani “new media & social media”.Sababu kubwa inayotajwa na wataalam ni kwamba vyombo vya zamani Radio,TV na Magazeti zimekuwa”merged” kwenye mitandao ya kijamii hivyo kufanya watumiaji wengi wa wategemee mitandao ya kijamii kupata habari za haraka na wakati japo suala la ubora linagonga vichwa vya wanahabari.
UHATARI WA VYOMBO VYA HABARI HASA SOCIAL MEDIA ZINAPOKOSA UTHIBITI.
Katika kuangalia madhara hasi ya vyombo vya habari kwa watumiaji hasa mitandao ya kijamii ambayo uthibiti ubora wa taarifa zake huwa ni mgumu kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu kinaitwa “gate keeping a & regulations” katika baadhi ya Nchi za ulimwengu wa tatu kama Tanzania.
Katika muktadha huo madhara ya mitandao ya kijamii kwa watumiaji inaweza kuelezwa vizuri kupitia madharia kuu mbili ambazo ni;
1.Nadharia ya vyombo vya habari kuwa ni kama bunduki na risasi”Magic Bullet theory”.Wataalam wa habari wanasema na kufananisha kuwa vyombo vya habari vina nguvu ya bunduki huku maudhui yake yakifananishwa na risasi kwamba endapo risasi inampata mtu inaweza kumuua.
Na ni hivyo hivyo kwa vyombo vya habari kwamba kama vitakuwa vinatoa habari za kupotosha vinaweza kuwafanya watu kuamini hivyo kuhatarisha amani na umoja wa kitaifa.
2.Nadharia ya pili ya jinsi ya ufanyaji kazi wa vyombo vya habari ni kwamba kupitia kitu kinaitwa”agenda setting”.Hii ni kwamba vyombo vya habari zikiwemo social media vina uwezo wa kukipa bania kitu fulani na baadae jamii ikaona kwamba ni kitu cha kweli hata Kama sio cha kweli!
Ajenda zinazowekwa na baadhi ya watu kwenye social media zinaweza zikaleta mfarakano na kuvunja umoja wa kitaifa kupitia njia ya agenda setting inayofanyika.Hii sio kitu ya kupuupwa kabisa.
Ufanyaji kazi wa nadharia hizi kuu mbili yaani “Media effects theories:Agenda setting & magic bullet theory” hapo juu uweza kuwa na madhara kama watumaji wa maudhui katika social media watakuwa na nia ovu kwa Taifa au kwa jamii zao!Hapa naongelea Facebook,you tube,whatup,intagram na mtandao wa Twitter.