

George Michael Uledi.
Kyela Mbeya.
November 1,2021.
Matamko kinzani ya Chama dola kwa Serikali yake yanaweza kuleta mambo makubwa mawili (I)kuibomoa na kuipunguzia uhalali Serikali kwa Wananchi wake na pili (ii)kuijenga CCM dhidi ya Serikali yake yenyewe lakini Chama kisipokuwa “strategic” katika kucheza na “situations”hizi, kinaweza kujikuta kinapotea kabisa kisiasa!
Dhana ya Chama dola kuisimamia Serikali yake haikwepeki lakini kukinzana kwa Serikali na Chama dola katika mambo madogo madogo kunaweza kuipotezea Serikali uhalali hivyo chama pia kukosa uhalali!
Gharama ya kuikosoa Serikali yako mwenyewe katika mambo fulani “publically” yanaonyesha kuwepo kwa “coordination failure”baina ya taasisi mbili hivyo kutukosesha uhalali kwa wapiga kura wetu!
Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndie Rais wa jamhuri na Mkuu wa Serikali lazima awe na uwezo wa kuzivaa kofia zote mbili kwa “political balance and indurance” ya viwango vya juu kabisa na kamwe hapaswi kufunikwa na Serikali yake wala hapaswi kufunikwa na Chama chake” game balancing”.
Matukio ya hivi karibuni ya chama kupingana na mipango ya Serikali hasa kuanzia kwenye suala la tozo za miamala ya simu na baadae CCM kuipongeza Serikali baada ya marekebisho katika viwango vya tozo za miamala ya simu inatupa picha mbili dhidi ya wapinzani na wananchi wetu!
Pia kitendo cha Chama dola hivi juzi kukinzana “publically” na Serikali kuhusu suala la kuamishwa kwa wamachinga na boda boda,kunatupa sura mbili ndani ya Serikali moja ya CCM!Kwa kifupi hii ni “tactical problem” na lazima chama changu CCM tuikwepe kufanya makosa kama haya!
NINI TUNAPASWA KUFANYA KATIKA SITUATION KAMA HIZI?
1.Makaripio na kauli kinzani za chama changu dhidi ya Serikali lazima yawe “closed door talks” kwa maana ya kwamba Serikali ya ccm inapaswa kukemewa kwa vikao na sio kwa kupitia “press conference” kila wakati!
2.Pili,hii haina maana kwamba chama kinapaswa kuwa bubu kwa Serikali yake,hapana!Chama kuja hadharani na kukinzana na Serikali maana yake ni kukidhana na Rais ambaye ndio mkuu wa Serikali na mwenyekiti wa Chama dola yaani CCM!
3.Tatu,Mkuu wa Serikali yaani Rais lazima sasa atusaidie kutoa”complete directives” kwa wateule wake kama Mawaziri Marc,Madc kwani ni wazi kuwa uwezo wa kila mteule wake haufanani na uwezo wa mamlaka ya uteuzi.
4.Kiongozi wa juu kwa maana ya mamlaka ya uteuzi lazima yajue uwezo wa wateule wake!Hipo hivi,mamlaka ya uteuzi lazima ijue dhana nzima ya “what & when to supervise ur followers and what & when not to supervise”.
Katika dhana nzima ya Uongozi,mamlaka ya uteuzi lazima ijue uwezo wa wateule wake na kuwepo kwa “taity & close directives”.Wapo wateule wenye uwezo wa kujisimamia lakini pia wapo wateule “slow learner’s”.Kuamini kuwa wateule wetu wote wana viwango sawa vya Uongozi ni kufanya makosa makubwa na inaweza kutugharimu safarini!
Kizuri zaidi,Mh Rais Samia Suluhu Hassan alishawahi kusema,nanukuu”….ndani ya Serikali kunakosekana kitu alichokiita “coordination”!Maneno haya aliyatoa wakati anamwapisha Katibu Mkuu kiongozi,Balozi Hussen Katanga.
5.Kudhani kuwa tutakuwa salama kwa kuipinga hadharani “makosa” yetu ya ndani wenyewe ni kujitafutia balaa kubwa mwaka 2025.Lazima CCM iwe na control na Serikali yake bila kuwa na “conflicting views” kuhusu maslahi mapana ya wapiga kura wake!
Wajibu wangu kwa CCM ni kulinda maslahi mapana ya CCM na Serikali yake ili tuendelee kukamata dola kwa miaka mingi mbele!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi zamani,Saut na University of Iringa na Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
+255746726484.