0 0
Read Time:47 Second

FROM GLASGOW TO COCO BEACH

DarEsSalaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan hajataka kupumzika, leo mchana ndio ameingia Tanzania akitokea Glasgow Scotland ambapo moja kwa moja amefika eneo la Coco Beach kujionea Vibanda vipya vilivyojengwa kwa kuzingatia mvuto na mandhari ya beach ambapo pia ameongea na Wafanyabiashara wa eneo hilo na kuongelea pia ya soko jipya la Kariakoo.

“Wote tunajua hali ilivyo Kariakoo Soko letu la Kimataifa Kariakoo limeungua lakini hatuwezi kuliacha hivihivi, Serikali, Wizara ya Fedha, TAMISEMI na Mimi tumehangaika tumetafuta fedha Bilioni 32 au Bilioni 34 tunakwenda kulijenga Soko la Kariakoo la Kisasa”

“Ramani ileile tuliyoachiwa na Waasisi lakini majengo ya kisasa ya yataingiza Wafanyabiashara kama 2000, watakaa kwenye nyumba kubwa safi watauza biashara zao vizuri, Waziri wa Fedha na TAMISEMI nataka kazi ya Karikaoo ianze mara moja kwasababu tumetafuta fedha na fedha zipo”

Rais Samia akiwa Coco beach jijini Dar es salaam,Leo Novemba 4,2021.

Video

KaziInaendelea

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %