0 0
Read Time:2 Minute, 34 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
January 19,2022.

Ni wazi kuwa kauli ya hivi karibuni ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kuwa “…ninajua kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake…”inaweza kuwa mwiba kwa watumishi wengi wa umma ambao wanataka kutafsiri kauli hiyo kama ruksa ya kufanya vitendo ya ufisadi na rushwa dhidi ya WANANCHI!

Nilitegemea taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa Nchini”Takukuru” kupitia kamanda wake mkuu,Kamanda Hamdan ingeshakuja na tamko na karipio kali dhidi ya wale wote wanaotaka kupotosha kauli ya Mh Rais na kutaka kurasmisha vitendo vya rushwa nchini.

Inawezekana kauli ile ya Mh Rais Mama Samia Hassan imetafsiriwa tofauti na watu wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii na kudhani kwamba Mh Rais ni kama katoa “go ahead” kwa watumishi wa umma kupiga “michongo” na “dili” zao kutokana na nafasi walizo nazo!

Kauli ya Mh.Rais ililenga katika kuwakumbusha watumishi wote wa umma Nchini kuwa waadilifu na wawajibikaji katika ofisi zao kwani mishahara pamoja na stahiki zao zingine zinatosha kabisa kuendesha maisha yao na hii NDIO maana halisi ya “…kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake..” ikiwa na maana kuwa kila mtumishi anapata kile anachostahili kupata na watumishi wa umma waachane na tamaa na ubinafsi zilizopitiliza!

Kauli ile ya Mh Rais iliwalenga Makatibu Wakuu wa Wizara ambayo alikuwa anazungumza nao siku husika ambao kimuundo wanapata mishahara pamoja na stahiki angalau zenye kuwawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku”….najua mnapata sana huko mliko lakini naona kuna wengine wanataka wavimbiwe kabisa…”

Tupenda kutoa tahadhari na onyo kwa watumishi wote wa umma wanataka kutumia vibaya kauli ya Mh. Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan kutaka kupotosha ukweli kuwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan, amehalalisha matendo ya rushwa na ubadhilifu kwa watumishi wa umma!Sio kweli!

Serikali ya awamu ya sita kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania yaani Takukuru, itaendelea kufwatilia kwa umakini na kwa ukaribu mkubwa nyendo zote za watumishi wa umma hasa wale waonadhani wanaweza kupotosha kauli ya Mh. Rais kwa maslahi yao binafsi!

Kuna taarifa za kuwepo baadhi ya askari wa usalama barabarani wanaotumia kauli ya Mh Rais kuweza “KUJUSTIFY” kuomba rushwa!

Tutegemee kuendelea kuona watu wengi zaidi wanaendelea kukamatwa kwa makosa ya rushwa sehemu mbalimbali nchini na kufunguliwa mashitaka ya rushwa kama uthibitisho na “commitment” ya serikali ya awamu ya sita katika kupambana na rushwa!Tusithubutu kutoa ama kupokea rushwa!

Serikali ya awamu ya sita ya chama cha mapinduzi chini ya Mh.Rais Mama Samia Suluhu Hassan, kupitia Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020 mpaka 2025 inabainisha kwenda kupambana na tatizo la rushwa kwa nguvu zote!

Mtu yoyote kwa nafasi yake yoyote atakayejaribu kufanya vitendo vya rushwa ama vitendo vya ufisadi wakati huu wa serikali ya awamu ya sita ni wazi kuwa atakwenda na maji!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa jeshi la Wananchi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

W

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %