George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
January 20,2022.
Tokea kijana Hamza mwaka jana afanye mauaji makubwa na ya kutisha, liliistua serikali yangu hasa vyombo vya ulinzi na usalama lakini matukio ya mauaji yanayoendelea Nchini katika kona mbalimbali ni kama tumeamua kuyapotezea kiaina!
Damu za watu wasio na hatia kuendelea kumwagika katika TAIFA kupitia mauji sio ishara nzuri sana na labda tunapaswa kuomba kwa iamni zetu mungu atuepushe na mauaji haya ya mara kwa mara katika ngazi ya familia!
Kuendelea kukaa kimya kwa vyombo husika bila kuja na tamko la nini tunafanya kunaendelea kuongeza hofu kwa taasisi ya ndoa na taasisi ya familia hivyo taasisi hizo mbili kukosa heshima ndani ya jamii zetu!
Gazeti la moja Nchini Tanzania kwa jina la Gazeti la Mwananchi mwishoni mwa mwaka jana lilibeba repoti ya uchunguzi wa kuwepo kwa wanaume wengi katika jiji la Dar es salaam wenye afya ya akili!Kama Dar es salaam kuna tatizo hilo basi kuna uwezekano wa tatizo hilo kuwa kubwa zaidi!
Nilitegemea serikali kupitia wizara ya Ustawi wa jamii wangeshatoka na kuja kutuambia mipango ya muda mfupi na mipango ya muda mrefu ya kukabili tatizo na kutuambia ukubwa wa tatizo lenyewe!
Pili nilitegemea Jeshi langu la polisi kuja na taarifa ya kina ya kiuchunguzi kutuambia watanzania hatua ambazo inachukua kukabiliana na tatizo hili kwa haraka maana huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine!
Wajibu wa Jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine ni kulinda raia na mali zao!Kulinda raia ni pamoja na kulinda uhai wa Watanzania dhidi ya matishio ya kutoana uhai na mambo yanayoendana na hayo!,Sijasikia popote kuhusu mipango ya Jeshi langu zaidi ya kutoa taarifa za matukio hayo!
Ni wakati sahihi sasa kwa Jeshi langu kuwekeza katika “social intelligence” katika ngazi ya familia ili kuweza “kudetect” matukio haya kabla ya kutendeka na hivyo kuchukua hatua “security preventive measures”.
Jeshi langu la Polisi lazima sasa liandae mpango wa haraka wa kuwashirikisha mabalozi wa nyumba kumi kumi kuweza kupata taarifa za siri katika maeneo yetu ili kuweza kuzuia utendekaji wa makosa haya!
Lakini wizara na idara mtambuka ambazo “zinadeal” na mambo haya kama mahakama na magereza lazima pia yaje na mipango yao katika kudeal na tatizo hili kwani kuendelea kutoa hukumu kali kwa watuhumiwa wa makosa haya ni kuendelea kujaza “vichaa”magerezani!
Nafasi ya vyombo vya dini pia lazima ichukue mkondo wake kwani moja ya chanzo cha mauaji haya ni imani za kishirikina!Wajibu wa dini ni kunyoosha mienendo ya watu wake,tunaomba wajibu huu utimizwe!
Tumechelewa sana kulitolea tamko tatizo hili na kuna siku itafika watu watakosa imani na taasisi ya familia na taasisi ya ndoa hivyo tutatengeneza Taifa la “mabachera” hivyo kuwa na taasisi ya familia isiyo imara katika Taifa!
Vyuo vikuu wajibu wake ni kufanya tafiti!Je,kuna tafiti zinaendelea kuhusu tatizo hilo?kama hakuna wajibu wetu ni upi kama taasisi za utafit?
Serikali kupitia wizara na idara zake lazima zitoke na kutuondoa hofu wananchi kwa maana hali sio nzuri sana!Kama mtu unayelala nae kitanda kimoja miaka nenda rudi anaweza kukuchinja je,usalama nyumbani kwako upo wapi?Tunaomba Serikali mtokea angalau mseme kitu!
+255746726484.