0 0
Read Time:1 Minute, 4 Second

WU® Media PRODUCTION LIMITED

Na Kagutta N Maulidi

BALOZI ASHANGAZWA NA UMATI MKUBWA WA WAUMINI WA KIISLAM

Balozi wa Tanzania Italy, Mh Mahamoud Thabit Kombo leo amesali Sala Eid El Fitri katika msikiti Mkubwa mjini Rome.

Balozi Kombo kwa mara ya kwanza amevutiwa na kushangazwa na umati Mkubwa uliohudhuria Sala ya Eid, mara tu baada ya kuondoleo vizuizi vya masharti ya Uviko 19.

Pamoja na ukubwa wa msikiti huo lakini Bado ilibidi Sala ya Eid isaliwe mara tatu ili kuhakikisha umati wote umepata fursa ya kusali Sala hiyo. Ikumbukwe Rome ndiko ulipo mji wa Vatican ambapo ndio makao makuu ya Baba mtakatifu wa Katoliki Duniani.
Baada ya Sala ambayo Mh Balozi alishiriki Pamoja na familia yake, alituma Salaam za mkono wa Eid kwa Watanzania wote wanaoishi Italy.

Katika Salaam hizo ambazo aliwatakia heri na baraka Watanzania wote na familia zao,Mh Balozi aliendelea kusisitiza umoja, upendo na ushirikiano baina yao Kupitia Jumuiya za Watanzania,aliwataka kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania na kulinda heshima ya Taifa lao. “Mwezi mtukufu ulikuwa ni mwezi wa kujitathmini kiimani na kuendeleza mazoea mazuri yanayotokana na mafundisho ya dini , hivyo ni wajibu wetu kuyaendeleza na kuishi kwa upendo bila kubaguana kwa imani au itikadi zetu” alimaza kwa msisitizo huo Mh Balozi wakati akituma salaam za Eid Kupitia Wabongo ughaibuni Media.

Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %