
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Generali Venance Salvatory Mabeyo Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo jumamosi tarehe 28/05/2022 ametembelea Ubalozi wa Tanzania mjini Rome Italy na kusaini kitabu Cha wageni.
Mkuu wa Majeshi amekutana na kuzungumza na wafanyakazi na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania mjini Rome Italy.
Mkuu wa majeshi yupo kwenye ziara fupi ya kikazi nchini Italia.
General Mabeyo ni mkuu wa majeshi wa nane kuteuliwa,aliteuliwa nafasi hiyo tarehe 6 February 2017 na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano Hayati Dr John Pombe Magufuli.









Picha kwa hisani ya:
Andrew C.Mhela
WU® MEDIA (ROME)