0 0
Read Time:1 Minute, 13 Second
JICHO LA ULEDI

NINI MAANA YA TAIFA KUWA NA WATU MILIONI SITINI KATIKA MAENDELEO YAKE?

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya.
November 1,2022.

I.Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mama Samia Suluhu Hassan,tayari leo imeweza kutambulisha soko jipya la bidhaa na huduma kwa Watanzania,kwa wana jumuiya ya Afrika Mashariki!

II.Ni zamu ya Wafabiashara wa huduma na bidhaa wa kitanzania sasa kuanza kufanya kitu kinaitwa “market segmentation” kujua wapi Soko linahitaji nini,mfano Iringa inahitaji nini leo,Mbeya,Katavi, Songwe na hata Dodoma!Watu Milioni 60 watahitaji kila kitu unachokijua!

Ni wakati wa Wakulima,Mabenki,Mashule , Hospitali,Usafiri na Wawekezaji wengine kujibu “demand”ya watu Milioni 60!Bonge la fursa kwa sasa!

III.Sekta ambazo kwa takwimu hizi zinonekana zinaweza kukua zaidi ni sekta ya Kilimo”Chakula”,elimu,afya,Usafirishaji na Umeme!Hii ni fursa kubwa kwa Taifa la Tanzania!Watu Milioni 60 angalau karibia 50% ya watu Milioni 69 watahitaji elimu,95% watahitaji huduma ya afya,100% watahitaji Chakula Kila siku ya Mungu!

IV.Takwimu hizi pekee yake zinaonyesha Tanzania inaweza kuwa Nchi Tajiri kwa kilimo,!Tanzania inaweza kuwa Nchi Tajiri kwa usafirishaji,Tanzania inaweza kuwa Nchi Tajiri kwa biashara ya ndani pekee yake!

Sijui Watanzania hawa wananielewa nini ni maana ya kuwa na Soko la ndani la watu Milioni sitini leo.Matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi, tayari imetambulisha fursa kubwa kwa production sectors!

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %