0 0
Read Time:2 Minute, 14 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 23,2022.

Repoti ya WIZARA kuhusu ajali ya ndege ya Precision iliyotokea Mkoani KAGERA hivi karibuni inatia doa sana kuhusu Utendaji kazi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania kwamba hatuko serious kivile!

“Moja ya kichekesho kikubwa ni kwamba Uwanja wa Ndege wa Bukoba hauna Control Tower kabisa miaka nenda rudi!

Unajua nini maana ya Control Tower katika ULIMWENGU wa Usafiri wa Anga?Hii ndio injini ya OPERATIONS Execution kwenye suala nzima ya Uongozaji Ndege kwa maana ya kutua na kupaa!Orders zote na kumwezesha rubani kupaa,kutua na hata kabla ya kutua akiwa angani ufanywa na Control Tower.

Jeshini au vitani kuna kitu kinaitwa Commanding Post au Operation Post!Achana na jeshini hata Mgodini kuna kitu kinaitwa Control Rooms!Majukumu ya kiulinzi au kiusalama uwa chini ya kituo hiki!Hauwezi kufanya Operations yoyote bila kuwa na Control Tower, Control Room au Commanding Post labda uwe mswahili tu hasa Mtanzania!

Maswali yangu ni angalau manne tu leo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania katika moja ya kipengele cha Control Tower/Control Room/Commanding Post ambacho at least nina uzoefu nacho wa kufanya kazi katika eneo la husika!

I.Mamlaka ya Viwanja vya Ndege watuambie haraka ni Viwanja vingapi havina Control Towers Nchini Tanzania na kwanini tunapeleka Ndege huko?,swali hili lazima lijibiwe haraka sana kabla ya madhara mengine makubwa kutokea!

II.Nani uwa anafanya Clearance kwa maana ya kumpa rubani taarifa zote za muhimu kuhusu hali ya Uwanja kwa wakati husika,hali ya hewa, runways,na Clearance zingine za muhimu Uwanjani na Angani?(kwa maana ya anga la landing site).

III.Kwahiyo rubani wetu walikuwa wana land mara zote kwa kubahatisha?kwahy hata ile Ndege ya ATCL ambayo iliamua kuondoa Ndege Uwanja wa Bukoba na kwenda kutua Mwanza Airport,ni wazi kuwa rubani wake alikuwa anajiongoza mwenyewe?

IV.Kwahiyo ile kauli”Official Statement” ya watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini ambayo walitoka baada ya ajali na kuwaambia Watanzania kuwa Uwanja wa Ndege za Bukoba ulikuwa salama sana ilikuwa na lengo gani?kumdanganya Mh. Rais?,kuwadanganya watanzania?,kumdanganya wasafiri?,hovyo kabisa!

NINI KINAFUATA SASA?

I.Nategemea kuanzia sasa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania mpaka dakika awe nyumbani!Meneja wa uwanja wa Ndege za Bukoba pia awe nyumbani kwa kushindwa kusema ukweli hasa baada ya tukio la pili la Ndege ya ATCL kushindwa kutua!

Kuna maswali mengi ya kuhoji lakini kwa maslahi mapana ya sekta husika na Taifa ni muhimu kunyamaza lakini angalau kuna watu wanapaswa kuchukuliwa hatua kuondoa uzembe na uswahili wa namna hii!

Jamani tuwe serious kidogo basi kwenye mambo ya msingi!Anga ni msingi wa Maendeleo ya biashara duniani kote.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
100 %