0 0
Read Time:1 Minute, 3 Second

Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza Wizara na Taasisi zote zinazohusika na maendeleo ya lugha ya kiswahili wawatumie vema wataalamu wa lugha hiyo waliopo nchini wakiwemo kutoka Vyuo Vikuu, Mabaraza ya Kiswahili na Vyama vya Kiswahili katika kukitangaza na kukibidhaisha kiswahili ili kitumike kama lugha ya ukombozi na kusaidia kuleta umajumui wa Afrika.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa balozi za Tanzania kuhakikisha zinaendeleza jitihada za kukuza na kufundisha Kiswahili katika ofisi za ubalozi na kuwashirikisha wadau wengine kama Diaspora na asasi nyingine zenye nia ya kukuza na kuendeleza Kiswahili.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 25, 2023) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Tuzo hizo zinadhaminiwa na Kampuni ya Mabati ya ALAF Limited – Tanzania ikishirikiana na kampuni ya Mabati Rolling Mills ya Kenya, chini ya uratibu wa Chuo Kikuu cha Cornell cha nchini Marekani.

“Muda mrefu imekuwa ikizoeleka kwamba lugha ya kiswahili inatumika katika masuala ya kitaaluma.

Lugha hii kwa sasa imeshavuka mawanda ya kitaaluma na inatumika katika nyanja za uchumi na biashara. Kwa kuzingatia ukweli huo leo tunashuhudia kwa macho yetu Kampuni ya ALAF ikitoa tuzo na ufadhili wa wanafunzi wanaosomea shahada ya umahiri katika Kiswahili.”

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %