
Rome, Italy 19/03/2023
Na Mwandishi wetu.

Commissioner General of Immigration TANZANIA Dr Anna Peter Makakala
Kamishna Generali wa Uhamiaji Dr Anna Peter Makakala kwa mara ya kwanza amekutana na viongozi na wajumbe wa Jumuiya za Watanzania nchini Italia siku ya jumapili tarehe 19/03/2023.

DR Anna Peter Makakala yupo Nchini Italy kwa ziara ya kikazi ambapo siku ya Jumamosi tarehe 18/03/2023 alikutana na Taasisi zisizo za kiserikali NGO ambazo zinafanyakazi zake nchini Tanzania. Katika mkutano wake huo uliohudhuriwa na mwenyeji wake Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA, Mh Mahamoud Thabit Kombo, aliweza pia kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kufanya kazi zao nchini Tanzania ikiwemo utaratibu wa vibali vyao vya Kazi. Kamishna jenerali pia amaeambana na Kamiashna wa uhamiaji Zanzibar ndugu Hassan Ali Hassan.
Katika mkutano aliokutana na Diaspora siku ya jumapili tarehe 19/03/2023 , Kamishna Jenerali aliweza kusikiliza taarifa kutoka kila Jumuiya za Watanzania nchini Italy zilizowakilishwa na viongozi wao. Mwisho katika taarifa alisikiliza risala maalumu ya kamati ya Diaspora iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora Italy Ndugu Kagutta N.Maulidi. Katika risala hiyo Mwenyekiti wa Diaspora alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupatia majawabu changamoto za Diaspora kama alivyo ahidi mara tu aliposhika Madaraka ya Urais. Mwenyekiti alisema tayari Benki kuu ya Tanzania imeruhusu Watanzania wenye uraia wa nje kufungua akaunti za Bank na kuwa hiyo ni matokeo chanya ya hatua zinazochukuliwa wakati mchakato wa sera ya mambo ya nje ukiwa katika hatua za mwisho. Mwenyekiti pia aligusia kuhusu Hadhi maalumu ambapo Dr Anna Peter Makakala alitoa ufafanuzi wa kina. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji aliwaasa Diaspora kutumia fursa inayotolewa na Ubalozi ili kuwa na Kumbukumbu nzuri ya mafanikio Kupitia falsafa ya Balozi Mahamoud Thabit Kombo “FALSAFA YA KUJIONGEZA KWA VITENDO” amesema kwa kuitumia falsafa hiyo watapata kujifunza mengi na Zaidi kufanikiwa. Mwenyekiti wa Diaspora alimpongeza na Kumshukuru Kamishna Jenerali kwa kukubali kuleta maafisa wa uhamiaji waliotoa huduma nzuri kwa weledi mkubwa kwa Diaspora Italy na Greece. Katika risala hiyo pia Diaspora wamemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwajali Diaspora wa Tanzania na kuwapa fursa mbalimbali sambamba na mkakati wa kutoa hadhi maalumu itakayowapa diaspora walio na uraia wa nje kuweza kupata haki mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwao kwa miaka mingi.
Mwisho Mwenyekiti wa Diaspora alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Italy kwa niaba ya Diaspora wote
Mgeni rasmi Pamoja na Balozi walitoa nafasi ya maswali na kuyatolea majawabu.
MATUKIO YA MKUTANO WA NGO NA UBALOZI AMBAPO MWAKA HUU MGENI RASMI ALIKUWA DR Anna Peter Makakala KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI TANZANIA









Sponsored by Equity Diaspora Banking
Equity Bank Tanzania
