
Khartoum, Sudan
WU® MEDIA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara yake ya mambo ya nje imeamua kuwaondosha wanafunzi wote wa kitanzania wanaosoma nchini Sudan kutokana na hali ya vita vinavyoendele nchini humo.
Kutokana na Hali ya kiusalama safari za ndege zimesitishwa nchini humo, hivyo wanafunzi hao wataanza safari yao kwa njia ya ardhini wakipitia mipaka ya nchi hiyo kuelekea nchini Ethiopia kwa usafiri wa basi, watakapo wasili nchini Ethiopia kwa ushirikiano wa balozi wa Tanzania nchini humo watapanda ndege kurejea nyumbani Tanzania.

Tuwaombee dua watoke salama na wafike nyumbani Tanzania salama.