
Na Mwandishi wetu,
Rome Italy
Sensei Rumadha Fundi amepokelewa Leo Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy baada ya kumalizika kwa semina ya kimataifa ya Sanaa ya Karate iliyofanyika mwaka huu Catania, Italia.


Katika ofisi za Ubalozi , Sensei Fundi alipolekewa na Mh. SIGFRIED NNEMBUKA kwa niaba ya Mh Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Kwa niaba ya Balozi Mh. Nnembuka amempongeza Sana Sensei Rumadha ambaye ni Mwalimu mkuu na Kiongozi wa Chama Cha Karate TANZANIA, Mh.Nnembuka amesema Balozi ametuma salamu za pongezi kwa kupeperusha Bendera ya Tanzania kwenye semina kubwa iliyoshirikisha walimu wa karate takriban 160 kutoka mataifa Mbalimbali Duniani. Mh Nenmbuka amesema kupeperusha Bendera ya Taifa ni heshima kubwa na ni fursa kubwa katika kuitangaza nchi , hivyo amemtaka Sensei kuendelea kuitangaza Tanzania kila anapohudhuria makongamano na hata kwenye mshindano ya kimataifa ya karate.
Mwisho Mh. Nnembuka amesema Ubalozi unafarijika Sana kuona Watanzania wanapokuja kutembelea Ubalozi wao na kusisitiza kuwa Ubalozi ndio nyumbani huku Ughaibuni.
Sensei Rumadha anatarajia kuondoka kesho Siku ya Ijumaa kureje nchini Marekani anakoishi baada ya kuwepo nchini Italy tangu tarehe 25/07/2023 ambapo semina ilianza tarehe 27/07/2023 na kuhitimishwa tarehe 30/07/2023.









