0 0
Read Time:2 Minute, 29 Second

WU® MEDIA

Rome Italy.

VIONGOZI WA JUMUIYA ZA ITALY KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAZIRI MAKAMBA PAMOJA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALY MH.MAHMOUD THABIT KOMBO

Waziri Makamba tarehe 29/01/2024 Jumatatu alikutana na wadau kwenye chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italy, hafla hiyo iliandaliwa ili wadau wa NGO’S na wafanya biashara wawekezaji pamoja na Diaspora waweze kukutana na Mh.Waziri.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiendesha hafla hiyo kwa mpangilio wa Ratiba akiwa yeye ndio mwenyeji

Kwenye hafla hiyo wafanya biashara walipata wasaa wa kuongea na Mh.Waziri na kuonyesha Nia kubwa ya kuongeza uwekezaji nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali. Wadau wa NGO’S nao walitoa ushuhuda na kueleza kazi wanazofanya nchini Tanzania , kwa mfano shirika moja ambalo limejikita kwenye kusaidia wenye mahitaji maalumu jambo ambalo linawafanya wahanga hao kuweza kufanya kazi zao za kimaisha kama watu wengine bila kuwa tegemezi.

Pamoja na wadau mbalimbali pia walikuwepo wageni waalikwa akiwemo balozi wa Italia nchini Tanzania ambae hufanya kazi kwa karibu sana na Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Diaspora ndio walipangwa mwisho kwenye ratiba kabla ya Mh. Waziri kuongea na wote ikiwemo kujibu maswali na changamoto za Diaspora.

Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Diaspora wakati akisoma Risala ya Diaspora

Risala ya diaspora iliyosheheni changamoto mbalimbali, ikiwemo uendeshaji wa jumuiya za watanzania Italia, lakini pia kuiomba serikali kuangalia uwezekano zaidi wa kuwashirikisha diaspora kwenye mambo muhimu ya kitaifa ili nao waweze kuchangia maendeleo ya nchi yao kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Katika kushirikishwa huko, Diaspora nchini Italia walimfahamisha Mh. Waziri kuwa kwa sasa hakuna taasisi yoyote ambayo ni mwakilishi wa Diaspora wote duniani, hivyo wameiomba serikali kupitia wizara husika kuangalia uwezekano wa kuunda shirikisho ambalo litatambulika na serikali, na kuwa ndio mwamvuli wa diaspora wa Tanzania duniani.

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Mh January Makamba ameahidi mbele ya diaspora kuwa yapo majawabu watakayo yafanyiakazi haraka na kuleta majibu kupitia ubalozi, lakini yapo mengine yanahitaji kuwepo na mazungumzo ili kuja na majawabu sahihi.

Kuhusu kuundwa kwa shirikisho, Mh Waziri ameahidi kuwa hilo ni muhimu na wanakwenda kulifanyia kazi, hivyo serikali itasaidia kuunda shirikisho hilo.

“Kuhusu shirikisho la diaspora tutasaidia kuundwa hilo msiwe na wasiwasi kabisa” Alisema Mh. Waziri Makamba.

Pamoja na yote lakini pia amesisitiza kuwa ipo miswada miwili ambayo inakwenda bungeni mwezi February na kila kitu kikienda kama ilivyopangwa basi mwaka huu 2024 ile hadhi maalumu itatoka.

Mh. Waziri akiongea na Diaspora mara baada ya kuongea na wadau wawekezaji na NGO’S

Diaspora katika risala yao pia wamempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipanga vyema safi yake ya diplomasia, sambamba na kumpongeza Rais pia diaspora Italy wamempongeza Mh. Waziri kwa kuaminiwa na Mh. Rais kuongoza wizara nyeti kwa maslahi ya Taifa.

Diaspora wameendelea kumshukuru balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia, Mh Mahmoud Thabit Kombo kwa kuwaalika na kuwapa nafasi nyingi za kujiongeza.

WAZIRI MAKAMBA AKIONGEA NA WADAU
Wageni waalikwa
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %