0 0
Read Time:56 Second

The Road to Paris

Na Nsangu Kagutta

Busto Arsizio Italy

Changalawe aliingia raundi ya pili baada ya kumtwanga bondia Pereira Diego wa Venezuela kwa KO siku ya tarehe 4/3/2024.

Kwa bahati mbaya matokeo ya leo siyo mazuri, tumepoteza pambano kwa majaji watatu kwa wawili, sipendi kutoa sababu japo ukweli tunaamini Mnorway amependelewa, lakini ndiyo ushindani. Tunashukuru kwa sapoti yenu, Mwenyezi Mungu awape afya njema, awalinde na kuwapa mafanikio katika shughuli zenu na maisha kwa ujumla“…..Alisema Makamu wa Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania Mh. Henry Benny Tandau wakati akiongea na Wabongo Ughaibuni Media.

Nae Coach Mohamed Abubakari Mohamed alisema bondia wake amecheza mchezo mzuri na kwa kweli hakutegemea kupoteza kwa sababu ya uwezo alioonesha tangu raundi ya kwanza mpaka ya tatu.

Wabongo Ughaibuni Media tunapenda kumpongeza sana bondia wa taifa kwa hari ,uwezo na uzalendo mkubwa alioonesha wakati akipeperusha bendera ya taifa,pongezi kwa mwalimu na mkuu wa msafara Makamu wa Rais wa kamati ya olympic Tanzania.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %