0 0
Read Time:42 Second

Geneva

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki na kufungua Kikao cha Kamati ya kuandaa Rasimu ya Azimio la matumizi ya Akili Bandia kwa mabunge chini ya Kamati maalum iliyoundwa kuandaa ya Azimio hilo, wakati Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani ukiendelea, CICG, Geneva, nchini Uswisi Leo tarehe 25 Machi, 2024.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewapongeza vinara wa Azimio hilo Mhe. Michelle Rampel Garner wa Canada na Mhe. Neema Lugangira wa Tanzania katika kuhakikisha kuwa IPU inakuja na Azimio lililo bora kuweza kukidhi uelewa na matumizi yatakayoonekana yanafaa kwa Mabunge na Jamii nzima.

Aidha, Azimio hilo litawasilishwa kwenye Bunge la pamoja pa IPU na kusomwa tarehe 27 Machi na kutarajiwa kupitisha rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa 150 utakaofuata.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %