0 0
Read Time:1 Minute, 5 Second

WU® MEDIA

Hadhi Maalumu kwa Diaspora

Serikali ya Tanzania inajiandaa kuwasilisha marekebisho kadhaa ya sheria za uhamiaji na ardhi za nchi hiyo wakati wa kikao cha Bunge cha bajeti ijayo. Marekebisho haya yanalenga kuwapa hadhi maalum Watanzania wanaoishi ughaibuni.

Katika mahojiano na gazeti la The Citizen hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Makamba aliangazia malengo makuu ya mapendekezo hayo ya marekebisho.

Jambo moja muhimu ni kutoa uhalali kwa watanzania walioko ughaibuni kumiliki mali ikiwemo ardhi ya Tanzania. Mabadiliko yaliyopendekezwa yangewapa uhuru wa kupitisha au kuhamisha mali kama wanavyoona inafaa.

Kipengele kingine muhimu cha hadhi maalum inayopendekezwa ni kurahisisha upatikanaji wa bima ya afya kwa familia za Watanzania wanaoishi nje ya nchi lakini na ndugu zao walio Tanzania.
Hatua hii inalenga kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya na usaidizi kwa wategemezi wa familia za diaspora nyumbani.

Zaidi ya hayo, serikali inakusudia kushughulikia taratibu za uombaji visa kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni ambao wana hati za kusafiria kutoka nchi nyingine.

Lengo ni kuhakikisha kwamba hawatwishwi na taratibu kali za uombaji visa kama raia wa kigeni wanapotembelea Tanzania.

Marekebisho haya yanalenga kurahisisha usafiri na kuimarisha uhusiano kati ya Watanzania walio nje ya nchi na nchi yao.

Waziri Makamba akiongea na Diaspora WA Italy alipokuwa kwenye ziara ya kiserikali mapema mwezi February.

Tanzania

Diaspora

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %