0 0
Read Time:36 Second

Bologna ITALY

Tangazo la msiba kutoka kwa Wanashirika wa Masista Watanzania Bologna Italy

Wapendwa wanajumuiya wote kwa niaba ya wanashirika wa masista watanzania tunawashukuru kwa matashi mema mliotutakia ukweli tunafarijika sana
Sista Stella alikuwa anaugua kwa takribani miaka 17, amefariki akiwa na umri wa miaka 46 katika hosptali ya Santa Orsola ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Hali ilizidi kuwa mbaya na kwa mapenzi ya Mungu usiku wa kuamkia jumapili Mungu alimchukua kwake.

Sista Stella kabla ya umauti haujamfika aliomba kuzikwa hapa nchini Italia na kwa kuwa shirika lina eneo la makaburi ambapo wanazikwa Masista wetu wote Le Budrie.

Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamisi Le budrie katika comune di San Giovanni mjini Bologna muda maalumu utatangazwa.

Asanteni kwa maombi yenu tuzidi kumwombea

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %