

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 8 Juni 2024 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa: Ethiopia, Zambia, Tanzania, Burundi, Qatar na Mauritania. Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu amejikita katika mambo makuu matatu: familia, matumaini na amani. Mababa wa Kanisa wanasema, Familia ni Kanisa dogo la nyumbani, shule ya upendo, udugu wa kibinadamu, huruma, haki na ukarimu. Mabalozi wawe ni alama ya matumaini na wajenzi wa amani!
vatican
BALOZI WA TANZANIA AWASILISHA HATI YA UTAMBULISHO VATICAN
Balozi wa Tanzania Mh Hassan Mwamweta amewasilisha Hati za Utambulisho (letters of Credence) kwa Baba Mtakatifu Francis. Hatua hii inampa uhalali wa kutekeleza majukumu kama Balozi wa Tanzania kwenye Ukulu Mtakatifu ( Holy See) mwenye makazi Berlin, Ujerumani.
Kwa muda mrefu Vatican kupitia “Roman Catholic Church”imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali nchini Tanzania. Miradi hii imegusa zaidi sekta ya afya na elimu

