0 0
Read Time:4 Minute, 33 Second

Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
May 24,2021.

JICHO LA ULEDI

Katika kujenga uchumi wa kisasa katika maeneo yetu ya kiutawala madhalani Wilayani unatakiwa uwe na faida kuu tatu ambazo zinaweza kukutoa katika hatua ndogo ya maendeleo kwenda hatua kubwa zaidi;

1.Kwanza,faida ya geografia”geographical competitiveness” inaweza kukufanya uwe Wilaya tajiri kama viongozi wanaweza kutafsiri faida hiyo na kuwa uchumi katika eneo husika.Wilaya ya Kyela inapakana na Nchi ya Malawi lakini pia Wilaya ya kyela ina bandari ya kuifanya iwe tajiri.

2.Utajiri wa rasilimali za madini au kilimo pia unaweza kukufanya uwe Wilaya tajiri hasa unapokuwa unalima mazao mkakati na yenye soko kubwa duniani!Wilaya ya Kyela imejaliwa kuwa na mazao muhimu ambayo unaweza kuuza sehemu yoyote duniani ambayo ni Cocoa,mawese na mchele!

Nani asiyejua mchele wa Wilayani Kyela jinsi unavyofanya vizuri sokoni katika majiji makubwa,nani asiyejua kuwa kilimo Cha mawese kingeweza kuleta utajiri mkubwa hasa wakati huu Nchi ikiwa kwenye uhaba na kuagiza mafuta ya kula toka nje ya Nchi.

3.Ukiwa na watu wenye akili kubwa ya kutafsiri fursa kuwa utajiri pia ni mtaji toka wa Wilaya kuweza kuendelea”Best brain & visionary leadership”.Akili zetu ndio utajiri wetu,uthubutu wetu ndio maendeleo yetu na zaidi watu wetu ndio utajiri wetu.

Kyela tunahitaji kuwa na viongozi wenye maono makubwa katika ngazi ya Wilaya hasa DC na Mkurugenzi wa Halmashauri basi.Watu wawili hawa wakishakuwa na maono na wakaweza kushirikiana Wilaya ya Kyela inaweza kuwa Wilaya au Halmshauri tajiri hata kesho wakitaka!

Ukiwa na faida moja kati ya faida hizo tatu kuu katika eneo lako unaweza kuwa tajiri na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika Wilaya yako na watu wako!Kikubwa viongozi lazima wawe na maono,washirikishe watu wao maono yao na mwisho wathubutu kutekeleza maono hayo kama timu,basi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %