
Na Mwanga Deogratius
Machi ya historia( Hakika Mtu Huyu Alikua Mwana Wa Mungu ) Mathayo 27 : 50 – 57
Nimeanza na Maneno ya Yule Akida ( Afisa ulinzi Kiongozi ) aliyekua na kikosi Cha askari wa kuhakikisha Yesu anasulubiwa Pale goligotha ! Baada ya kushuhudia Giza la Saa Sita Mchana lililodumu kuliko lile la kupatwa Kwa jua ‘ na kuchanika Kwa Pazia la hekalu vipande viwili Vizito litenganishalo pahala patakatifu na patakatifu Zaidi , Kufunuliwa kwa makabuli na watakatifu kuwatokea Watu Wengi mjini , kupasuka kwa Miamba na hekaheka zote zilizo waarifu Wayahudi Kwamba torati inapata Utimilifu
Hayati Daktari JPM Hakika Alikua Mwana Wa Mungu Kama Mathayo 27 ; 50 – 57 inavyosema ‘ Ukitizama Ule Umati wenye Majonzi Makubwa pale Uwanja Wa Taifa Temeke Siku ya Kuagwa Kwake Na Watanzania , Achilia Mbali ile picha iliyojizolea Umaarufu Ya Kijana Aliyepiga Saluti Mbele ya gari Maalumu lilokuwa likiukokota Mwili wa Hayati Daktari Magufuli , mamia ya waombolezaji barabarani wakiongozwa na kina mama waliokuwa wakitandika vitenge na maua barabarani unakopita Mwili wa Rais Magufuli Utakubaliana nami kutumia Maneno ya Yule Akida Si Kwa Yesu Sasa Bali Kwa Magufuli
Je Magufuli ni Kama Mussa ? Ambaye mbali Na kutumia miaka Mingi Kuwatoa Utumwani Misri Kwa Farao Na Kupambana Na changamoto za Jangwani na Wana Israeli hakufanikiwa Kuifikia Nchi Ya Ahadi ? na baadae kufa katika milima ya moabu Baada ya kuonyeshwa na Mungu Nchi iliyojaa maziwa na asali ( Kumb 34 . 5 )
Picha ya video pale Uwanja wa ndege wa Kimataifa Wa Julius Nyerere ikionyesha mamia ya waombolezaji wakivunja Uzio , kuingia ndani wakiizonga ndege yenye Mwili wa Rafiki Yetu Ndg John Pombe Magufuli Kwaajiri Ya Safari ya Kijijini Chato Ilihakisi Kazi Nzururi alizowafanyia Watanzania ambao kwa wakati huo hawakuwa wakiamini kilichotokea
Katika kipindi Chake Cha Uongozi Tanzania imepata mwelekeo Mpya , miradi mingi ya kujenga uchumi endelevu imeanza kutekelezwa mradi Mkubwa wa Umeme wa ndoto za Mwalimu Nyerere ( stieglers gorge ) utakaogharimu dola za kimarekani 2.9 billioni sawa na takribani trillioni Sita Na nusu za kitanzania umeanza kutekelezwa , Reli ya kisasa Toka Dar Es Salaam mpaka Isaka Kahama Kuelekea Rwanda Mradi wa 2.2 billion dola umeanza kutekelezwa Katika kipindi Chake Cha awamu ya Tano
Tunapo sherehekea Miaka 60 ya UHURU wa Nchi Yetu hatuna budi kukumbuka Mchango wa mpiganaji huyu Toka Chato ,miradi ya Afya iliyotekelezwa Ni mingi ( Vituo vya Afya , Hospitali za Wilaya na Kanda ) Nchi nzima , Elimu Bure Kwa msingi na sekondari Miradi ya nishati ( REA ) na ujenzi wa miundombinu ya Barabara Vilikua Moja ya vipaombele Katika serikali yake
HAUKUA MWAKA RAHISI Tunamshukuru Mungu Kwa Zawadi ya Maisha ya JPM Mungu ampe Pumziko la Milele AMINA
KAZI IENDELEE
Mwangoka Deogratius








