
Na Mwandishi wetu
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
“MacFrut 2022” RIMINI ITALY

Leo Jumatano tarehe 4 May ,2022 ,Ubalozi wa Tanzania umeshiriki onyesho kubwa la Kimataifa la “MacFrut 2022″ linaloendelea mpaka tarehe 6/05/2022 katika mji wa RIMINI nchini Italia.
Balozi wa Tanzania Nchi Italia Mh.Mahmoud Thabit Kombo aliongoza washiriki wote wa Tanzania wa sekta ya kilimo Kupitia wizara ya kilimo iliyo wakilishwa na Mkurugenzi wa wizara Ndugu Beatrice pamoja na Benki ya kilimo Tanzania.
Jukwaa la Tanzania liliweza kuwa kivutio kikubwa kutokana na Bidhaa zake mbalimbali zilizo onyeshwa kwenye Maonesho hayo makubwa yaliyo hudhuriwa na zaidi ya nchi sabini na Saba (77) Duniani.
Kivutio kikubwa katika Maonesho hayo kwa upande wa Banda la Tanzania ilikuwa ni Mazao ya Parachichi, Kahawa, Viungo na Korosho za Tanzania.
Kampuni kadhaa zilizotembelea Jukwaa ama sehemu ya maonesho hayo kwa Upande wa Tanzania zilionesha nia ya kutaka kuingia mikataba ya uagiziaji wa mazao hayo nchini Italy na Bara la Ulaya (European Union).
Kwa upande wa Tanzania Kampuni mbili kuu zilizoongoza katika Bidhaa hizo ni EatFresh Pamoja na Bri.
Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo, alipokuwa akizungumza na Mwandishi wetu,amesema ushiriki wa Tanzania katika makongamano ya kibiashara na maonyesho ya kimataifa ya kibiashara ni moja ya mikakati ambayo kwa kushirikiana na maofisa wake wa Ubalozi wanatekeleza sera ya Diplomasia ya Uchumi, ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan. Balozi ameahidi kuwa wataendelea kuhakikisha ushiriki huu unakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na kufungua milango ya kibiashara Zaidi.