
Tanzania ilikuwa mbele ya Muda
Anaandika Dr. Yahya Msangi .
Miaka mitatu iliyopita wakati Balozi #Mulamula kakalia Kiti Cha Waziri wa Mambo ya Nje kulizuka vuguvugu kubwa miongoni mwa diaspora.

Diaspora tuliandaliwa mkutano, vipeperushi na dodoso ambalo maudhui yake yalikuwa kuhamasisha diaspora tudai uraia pacha.
Ilikuwa ukipinga inaonekana diaspora mkorofi. Lakini baadhi yetu tulisimama imara licha ya upinzani kuwa mkali. Nakumbuka kwenye kikao kimoja ambacho Balozi Bana alihudhiria na tuliunganishwa na “wataalamu” toka Tanzania Kwa njia ya mtandao mimi nilihoji:
- Ni nani kati yetu ambaye ameenda kuwekeza Tanzania akakataliwa Kwa kuwa hana uraia pacha ?
- Nani kati yenu ana mtaji wa kutosha kuwa mwekezaji Tanzania? Mbona karibu wote wazamiaji ?
- Nani ambaye kaoa huku nje na alipoenda na mkewe na watoto walizuiwa Kwa kuwa sio raia wa Tanzania ?
- Mnaweza kunieleza kwa Nini wawekezaji wa kigeni ambao wengi hawana uraia pacha wao wanawekeza Tanzania lakini nyie mnadai mnazuiwa? Mbona hamna huo uraia lakini mko huku nje mnaganga njaa? Mbona hamfukuzwi Kwa kuwa hamna uraia pacha ?
- Hivi uraia pacha faida yake kwetu ni nini haswa ?
Basi madodoso yake yalitumwa Wizarani. Mnadai ya uraia pacha yakaenda baada ya Mama Balozi kuondoka.
Enzi zile Kila mashabiki wa uraia pacha alidai Marekani upo. Ni kweli. Ila ulikuwa unawatesa. Na Sasa Seneta wa Ohio Bwana Bernie Moreno kapeleka msaada wa kutaka uraia pacha ufutwe Marekani. Anapendekeza pawepo na “Exclusive Citizen Act of 2025 unaweza SEMA ” Sheria ya uraia mmoja tu ya mwaka 2025 “.
Sheria hiyo itapiga marufuku raia wa Marekani kuwa na uraia wa nchi nyingine. Na ikipitishwa na senate raia wenye uraia wa nchi nyingine watapewa mwaka mmoja tu kuamua ni uraia upo wanataka. Mwaka ukipora na ukawa hujaamua utahesabika umejivua uraia wa Marekani.
Na ikatokea huko baadae ukagundulika una uraia wa nchi nyingine basi hata kama ulidai una uraia wa Marekani utahesabika hukuwa raia wa Marekani toka siku ulipochukua uraia wa nchi nyingine. Na maslahi yote uliyopata katika kipindi hicho utatakiwa kuyarejesha.
Huu ni mtihani mkubwa kwa wenzetu wa diaspora. Lazima EU na wengine nao wataiga.
Sasa diaspora watatakiwa waamue wanataka uraia upi? Ngonjera ya uraia pacha itakufa natural death.
Tuchukulie wewe ni diaspora uliyekikita kutukana nchi ambayo ndio raia Kwa sababu tu una uraia wa huko uliko? Utakapochagua uraia wa Marekani (kwa mfano) kuanzia hapo hapo utalazimika kuomba visa utakapotaka kuja Tanzania kwa shughuli yoyote ile! Utatakiwa ulipe ada ya visa kwenda kwenu kuwaona wazazi, ndugu na jamaa. Passport yako ya Tanzania itakuwa haipo Tena kwenye mtandao wa Uhamiaji. Na utakapokuwa Tanzania kuna huduma utazikosa kwa kuwa hutahesabika kama raia.
Diaspora kazi inataka kuanza. Tutachagua wewe ni ndege au mnyama?
Nampomgeza Seneta Bernie Moreno kwa kukusudia kukata mzizi wa fitna.








