0 0
Read Time:1 Minute, 24 Second

Korea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo amewasili katika Jamhuri ya Korea Mei 30, 2026 kwa ziara ya kikazi pamoja na kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea na Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 31 Mei 2026 hadi 02 Juni 2026 jijini Seoul nchini Korea.

Mara baada ya kuwasilili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon, Mhe. Balozi Dkt. Kombo alipokelewa na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea, Mhe. Noel Kaganda na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea.

Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Kombo alitembelea Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo aliongoza kikao cha kupokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano na ziara hiyo kwa ujumla iliyowasilishwa kwake na Balozi Kaganda pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Ausralasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Felista Rugambwa. Ujumbe wa Tanzania unamjumuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha-Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

Vilevile, wakati wa ziara yake, Mhe. Waziri Kombo pamoja na mambo mengine atakutana na Wafanyabiashara wakubwa wa Korea, atazungumza na Diaspora wa Kitanzania wanaoishi Jamhuri ya Korea pamoja na kufanya mikutano ya Uwili na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mhe. Cho Hyun.

Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Korea na Afrika 2026 utahusisha program mbalimbali ikiwemo Mkutano wa Maafisa Waandamizi, vikao vya pamoja vya Mawaziri wa Mambo ya Nje, mikutano ya pande mbili, Jukwaa la Biashara la Korea–Afrika pamoja na ziara za maeneo mbalimbali zitakazolenga kuimarisha ushirikiano wa kiserikali na mahusiano baina ya watu wa pande zote mbili.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %