0 0
Read Time:1 Minute, 57 Second

Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia leo tarehe 25 Januari, 2021 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini ambapo amepokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa ndege wa Chato, uliopo mkoani Geita. Baada ya mapokezi ya kitaifa Mhe. Zewde na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Mgufuli waliambatana kwenda kuendelea na ratiba ya mazungumzo baina yao, na baadaye wote kwa pamoja walijitokeza kuelezea umma wa Watanzania kupitia waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yaliyojili na kukubaliana katika mazungumzo hayo.Rais Magufuli kwa upande wake ameelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali kupitia ushirikiano na uhusiano mzuri uliodumu kwa muda mrefu  baina ya Nchi hizi mbili ikiwemo katika sekta ya biashara na uwekezaji. Mhe. Rais ameeleza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni biashara kati ya Tanzania na Ethiopia imeendelea kuimarika madhalani, kwa mwaka 2016 biashara ilikuwa bilioni 3.07 na kufikia bilioni 13.55 kwa mwaka 2019/2020. Vilevile miradi 13 yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 14.57 kutoka nchini Ethiopia zimesajiliwa nchini kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %