2 0
Read Time:2 Minute, 24 Second

Na Mwana Habari wetu

H.Jiwe Ascoli Piceno IT.

WU® MEDIA

Diaspora wa Tanzania nchini Italy wamesherehekea miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.

Meza kuu

Sherehe hizo zimefanyika siku ya Jumamosi tarehe 29/04/2023 mjini Ascoli Piceno ambako ziliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania ya Ascoli. Maandalizi haya ni muendelezo wa utaratibu uliowekwa na Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Yeye kama mlezi aliamua kuwa sherehe za Muungano na zingine za kitaifa zitakuwa zikifanyika kwa awamu na kuandaliwa na Jumuiya za Watanzania wa sehemu husika.

Nia ya Balozi kufanya mzunguko huo wa uandaazi wa sherehe za kitaifa ni katika kutoa fursa kwa Diaspora nchini Italia kuweza kujiongeza na kutafuta fursa mbalimbali kwa kushirikisha serikali za maeneo wanayotoka katika dhana Ile Ile ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Diplomasia ya Uchumi Kupitia Diaspora.

Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alikuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy,Mh Mahmoud Thabit Kombo akiongozana na Mkewe Mama Zakia Kombo. Pamoja nao waliokuwepo pia Maofisa wa Ubalozi na HOC Madam Jubilata Mgaya.

Maofisa wa Ubalozi walihudhuria wakisikiliza kwa makini historia ya Muungano wakati Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiongea

Wageni waalikwa , alikuwepo Meya wa mji wa Castel di Lama (Sindaco) Dott. Mauro Bochiccio Pamoja na Baba Askofu wa Ascoli Piceno S.E.R Mons, Gianpiero Palmieri.

Mwenyekiti wa Jumuiya Watanzania ya Ascoli Piceno dada Anna Minja ambae ndie alikuwa mwenye dhamana ya kusimamia kuaanda sherehe hiyo , aliwapa nafasi Wageni kutoa salaam zao fupi. Meya wa Castel di Lama na Na a Askofu walimshukuru Balozi wa Tanzania kwa kuwaalika Kupitia Jumuiya ya Watanzania Ascoli Piceno. Wamesema kwa kufanya hivyo wanaamini ni mwanzo wa mashirikiano baina ya Watanzania na wenyeji lakini pia kutoa nafasi ya fursa mbalimbali kwa nchi zote mbili.

Mwisho Mwenyekiti Anna Minja alimkaribisha Mgeni Rasmi.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo baada ya shukran kwa waalikwa alitoa historia ya Muungano wa TANZANIA, sambamba na mashirikiano ya kibiashara baina ya nchi mbili. Balozi aliwashukuru Diaspora kwa kuendelea kujiongeza kwa vitendo, na kuwataka waendelee kumuunga mkono Rais Samia hasa kwenye diplomasia ya Uchumi wakishirikiana na Ubalozi. Balozi pia amewakikishia Diaspora wote nchini Italia kuwapa ushirikiano zaidi kwenye kila jambo lenye tija kwao na kwa Taifa.

Sherehe iliendelea na ratiba zake , na baada ya Chakula na vinywaji kulikuwa na burudani ya mziki wa Kitanzania na kunogeshwa zaidi kwa show Kali ya Msanii wa Kizazi kipya anaeishi nchini Italy kwa sasa Hussein Machozi

Balozi katika picha akiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Ascoli Piceno Anna Minja na Binti yake Abbia Maswi ambaye ni professional MakeUp Artist
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ascoli akiwa na Mama Zakia Kombo
Mke wa Balozi Mama Zakia Kombo akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia (c) Sig.ra Judith Joseph na katibu wake dada Cecilia Lemmah
Mwenyekiti Madam Anna Minja
Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %