0 0
Read Time:47 Second

29 Agosti, 2024 | Brazzaville, Congo
Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile; afanya kikao na Waziri-Afya, Wabunge na Mabalozi, Atoa neno la Shukrani

Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama pembezoni mwa Mkutano wa 74 wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, unaoendelea Jijini Brazaville, Congo.

Kwenye Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mabalozi na Maafisa Waandamizi wa Wizara za Afya na Mambo ya Nje, Dkt. Ndugulile ametoa shukrani za dhati kwa kuhitimiisha salama Kampeni za Uchaguzi na kupata ushindi mnono kwa Tanzania. Aidha kupitia mkutano huo amewaahidi watanzania kuto kuwaangusha.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya ambaye ndiye aliyepiga kura ya Tanzania kwenye uchaguzi huo uliofanyika tarehe 27 Agosti 2024, amempongeza tena na kumsihi kujipanga vizuri na timu mahiri kwa kazi

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %