
Hanoi Vietnam
Tanzania na Vietnam zimekubaliana kuanzisha ushirikiano wa sekta binafsi ili kuchagiza kasi ya ukuaji wa biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamefikiwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika leo Aprili 29,2025 kati ujumbe wa Tanzania na Vietnam uliojumuisha wafanyabishara na viongozi wa sekta binafsi kutoka pande zote mbili yaliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Chemba ya Biashara na Viwanda ya Vietnam jijini Hanoi.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo umeongozwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Kombo.
Miongoni mwa fursa zilizopata mwitikio mkubwa zaidi miongoni mwa wafanyabishara hao ni pamoja na zao la mkonge, vifaa vya ujenzi, uchumi wa buluu, madini hadimu na teknolojia ya habari na mawasiliano
Kwa upande wake Waziri Kombo amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi imara wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango na nafasi ya sekta binafsi kwenye maendeleo ya Taifa hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa sekta binafsi ili kuongeza tija zaidi.











