0 0
Read Time:50 Second

Dar Es Salaam , TANZANIA

Rais Samia ampokea Rais Chapo Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkaribisha mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Msumbuji Mhe. Daniel Chapo katika Ikulu ya Dar es Salaam Mei 8, 2025.

Rais Chapo amefanyiwa mapokezi rasmi yaliyoambatana na kupigiwa mizinga pamoja na kukagua gwaride la heshima na kisha kusaini kitabu cha wageni mara baada kuwasili Ikulu.

Viongozi hao wamefanya mazungumzo ya faragha yatayofuatwa na mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari pamoja na kusainiwa kwa Mikataba miwili (2) na Hati za Makubaliano nne (4) katika sekta mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati Tanzania na Msumbiji.

Ifahamike kuwa Tanzania na Msumbiji zina ushirikiano wa kidugu wa muda mrefu. Chama tawala cha Msumbiji, FRELIMO kiliasisiwa Tanzania huku wapigania uhuru wa Taifa hilo kwa wakati huo ambao ni pamoja na Samora Machel na Eduardo Mondlane wakiifanya Tanzania kuwa hifadhi salama.

Katika ziara hii ya siku tatu, Rais Chapo atatembelea mradi wa SGR pamoja na kufanya ziara Zanzibar.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %