
Kampala UGANDA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe maalum, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili jijini Kampala Uganda na kupokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Simuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe tarehe 12 Mei, 2025.
Waziri Kombo anatarajiwa kuwasilisha Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jenerali Yoweri Kaguta Museveni.




