
Abijan IVORY COAST
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) amewasili nchini Ivory Coast kumwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Siku mbili wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Afrika unaoanza leo Mei 12, 2025 jijini Abidjan.
Mhe. Majaliwa amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Félix-Houphouët-Boigny Jijini Abidjan na Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Mhe. Robert Beugre Mambe.



