0 0
Read Time:49 Second

VATICAN

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Vatican mwenye makazi jijini Berlin, Ujerumani, Mhe. Hassani Iddi Mwamweta, amewasilisha salamu za pongezi na kheri za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Baba Mtakatifu Leo wa XIV.

Kwenye salamu hizo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Papa Leo XIV kufuatia kuchaguliwa kuwa Papa wa 267 na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani. Sambamba na salamu hizo, Mheshimiwa Rais amemuahidi Papa Leo wa XIV ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa upande wake Papa Leo XIV ameeleza furaha yake kupokea salamu kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi ambayo anaipenda na amekuwa akiitembelea. Ameeleza pia utayari wake wa kufanya kazi kwa karibu na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika.

Mazungumzo hayo yamefanyika mara baada ya sherehe ya kusimikwa rasmi kama Rais wa Vatican na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV yaliyofanyika leo Mei 18 katika Basilika la Mt. Petro, Vatican.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %