0 0
Read Time:1 Minute, 1 Second

Dar Es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo(Mb.), ameshiriki katika Mhadhara wa Siku ya Afrika(African Day Lecture) uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amezitaka nchi za Afrika kutambua utajiri mkubwa wa Afrika katika Uchumi wa Buluu na madini unaohitaji nguvu ya pamoja ya Waafrika ili kuweza kuwanufaisha watu wake.

Katika Mhadhara huo ulioandaliwa na Taasisi ya Thabo Mbeki kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Kombo amesisitiza kuwa Afrika ina utajiri wa Bahari ambapo wanaowekeza zaidi kwenye uchumi wa buluu ni watu kutoka mabara mengine mbali na Afrika na hivyo fedha nyingi kwenda nje.

Aidha, ameeleza kuwa sekta ya madini barani Afrika, inachangia sehemu kubwa ya mapato ya mataifa ya Afrika huku uchakataji wa madini ya kimkakati kama vile nikeli na titanium pamoja na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na rasilimali hiyo nyingi ikitoka nje. Amewasihi Waafrika kuwekeza katika sekta hizo mbili ili kudhibiti na kufaidika na rasilimali hizo.

Kwa upande wake, Balozi Ami Mpungwe amesema kuwa, ili rasilimali hizo ziweze kuleta matokeo bora zinahitaji usimamizi mzuri huku akisisitiza kuwa, msingi wa kuyafikia maendeleo endelevu ni kuhakikisha suala la amani, umoja na mshikamano linapewa kipaumbele kikuu.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %