
Na Kagutta Maulidi
Mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi 2025
Mkutano mkuu Maalumu wa chama cha mapinduzi ulioanza tarehe 29/05/2025 na kuhitimishwa tarehe 30/05/2025 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkutano huo chini mwenyekiti wake Dkt. Samia Suluhu Hassan ulihitishwa kwa kuzinduliwa rasmi ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2025-2030.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wageni wawakilishi kutoka vyama vya siasa mbalimbali Duniani. Pamoja na wageni waalikwa kutoka balozi mbalimbali nchini Tanzania lakini pia walikuwepo Diaspora kutoka nchi sita. CCM Diaspora waliwakilisha salamu za pamoja ,shukrani na pongezi kwa Chama na serikali. Salaam ilisomwa na ndugu Eva Nangela Diaspora kutoka nchini Italy kwa niaba ya Diaspora wote.
CCM diaspora wamemuahidi Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa watashiriki katika kampeni wakati utakapowadia kuhakikisha Chama chao kinapata ushindi wa Kishindo Tanzania Bara na Zanzibar na kuwa wanaposema Samia mitano Tena huwa Wanamaanisha. Diaspora wamempa zawadi Rais Samia na Rais Mwinyi kama ishara ya upendo kwa viongozi wao.

Mwisho Rais Samia aliwashukuru sana kwa uzalendo na upendo kwa nchi na Chama chao, na kuwataka kuisemea nchi huko ughaibuni mara wanapotokewa wengine kupotosha.
CCM diaspora waliohudhuria ni kutoka UK, USA, ITALY, DENMARK , URUSI ,NORWAY NA FINLAND




















