
WU®Media
Dodoma Tanzania
Watanzania wanaoishi nje yaani ughaibuni maarufu kama Diaspora, leo Jumatatu 2/06/2025 wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata mualiko maalumu.

Diaspora hao ambao ni kutoka matawi ya Chama cha Mapinduzi ya nje walihudhuria mkutano mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika tarehe 29/05/2025 mpaka tarehe 30/05/2025.
Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutambua mchango wa Diaspora kwenye maendeleo ya nchi kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Diaspora hao ambao wanaondoka leo kurejea Dar Es Salaam kwa Treni ya SGR pia wamepata mualiko kutembelea Zanzibar.







Kwenye viunga vya Bunge


