0 0
Read Time:1 Minute, 2 Second

Na Kagutta N.M

Zoezi laendeshwa kwa kwa siku mbili

Ubalozi wa Tanzania nchini Italy umeendesha zoezi la uandikishaji Diaspora wa Tanzania kwenye mtandao wa Diaspora Digital Hub. Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki imetenengeneza mfumo wa usajili kwa Diaspora wote wenye lengo la kuwa na kumbukumbu zitakazowezesha kujua idadi ya Watanzania Ughaibuni, taaluma zao na ujuzi.

Serikali ipo katika hatua za awali za kuweka njia bora za kushirikisha diaspora kwenye fursa mbalimbali zilizopo nchini lakini pia waweze kushiriki katika maendeleo ya nchi yao kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Zoezi liliendeshwa kwa ushikiano wa ubalozi na kamati kuu ya Diaspora lakini Jumuiya ya Watanzania Italia – Napoli mkoani Campania. Afisa wa Ubalozi ndugu Siegfried Filipo Nnembuka alisimamia zoezi hilo kwa ushirkiano na maafisi wengine wawili Ndugu Joseph Tarimo na Ms. Jacqueline Mbuya. Wakati wa kufunga zoezi hilo ndugu Nnembuka aliongea kutoa shukrani kwa kamati kuu ya Diaspora na Jumuiya ya Watanzania kwa kufanikisha zoezi, pia aliwashukuru Watanzania wote waliojitokeza kushiriki zoezi hilo na kuwataka kufikisha ujumbe kwa wengine ili wajue umuhimu wa kujiandikisha kwani hata serikali inapotaka kuondoa raia wake inapotokea majanga inakuwa rahisi kujua idadi ili kuweza kufanikisha taratibu hizo, alisema ndugu Nnembuka.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %