1 0
Read Time:1 Minute, 21 Second

Na Kagutta N.M

Ubalozi wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Roma washiriki kuandaa mdahalo wa siku ya kiswahili duniani

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchi Italia umeshiriki na kuongoza wadau mbalimbali katika mdahalo kuadhimisha siku ya kiswahili duniani. Mdahalo huo ulifanyika leo siku ya jumatatu tarehe 07/07/2025 Castelfranco Emilia katika mji wa Modena.

Ubalozi ukishirikiana na taasisi za diaspora wa Tanzania za Shamrashamra na Goirgio Marincola,ulihitimisha maadhimisho hayo kwa mdahalo uliohudhuriwa na wadau mbalimbali waliofika Castelfranco Emilia lakini pia Ubalozi ulitoa fursa kwa washiriki walio mbali kushiriki kwa njia ya mtandao wa zoom.

Katika madhimisho hayo makubwa yalihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Castelfranco Emilia Mh. Giovanni Gargano na upande wa ubalozi uliwakilishwa na Kaimu mkuu wa kituo Ubalozi wa Tanzania jijini Roma Mh. Eva Kaluwa ambae aliambatana na Afisa anaeshughulikia masuala ya Utamaduni siasa, Lugha na Diaspora kwa ujumla ndugu Sigfried Nnembuka.

Ubalozi wa Tanzania na jiji la Castelfranco Emilia wamekubaliana kuwa na mikakati ya mashirikiano katika sekta mbalimbali kwenye diplomasia ya uchumi lakini pia kwenye Utamaduni ambapo lugha ya kiswahili imo kama sehemu ya utamaduni. Makubaliano hayo yatakamilika baada ya mchakato wa kusaini Mou..” Alisema kaimu mkuu wa kitu Ms. Eva Kalua”

Meya wa jiji la Castelfranco Emilia alifurahishwa sana na tukio la maadhimisho ya kiswahili ambapo alisema yuko tayari kutoa ushirikiano ili kuendeleza harakati hizi za kukuza lugha ya kiswahili na kukibidhaisha kwani lugha ni njia kuu ya mawasiliano inayopelekea mashirikiano zaidi baina ya jamii, kitamaduni,siasa na uchumi.

Maadhimisho haya yalianza tangu tarehe 5 na kuhitimishwa leo tarehe 7/07/2025

Photo/video by Jiwe Msawira for Wabongo Ughaibuni Media.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %