
WU®Media
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt.Justin H. Ringo na baadhi ya maafisa wa ASA wakiwa na wawekezaji wa kilimo kutoka Nchini Italia wakiangalia vipando katika maeneo ya maonesho ya nane nane katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Wawekezaji hao wameridhishwa na Maendeleo ya kilimo hapa Nchini pamoja na kuona fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Aidha ugeni huo umefurahishwa na maonesho ya Nane nane katika vipando vya ASA hasa kwa kuona mazao mbali mbali yakiwa katika hali nzuri yenye ustawi na mpangilio mzuri.
Mashirikiano hayo yameletwa na ziara ya katibu Mkuu wizara ya kilimo Mh.Gerlad Mweli alipofanya ziara ya kikazi Nchini Italia kuangalia fursa za kilimo.








