2 0
Read Time:1 Minute, 15 Second

WU®Media | Na Kagutta NM

Mchango wa Diaspora katika Diplomasia ya uchumi | Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italia (IN CAMPANIA) wapokea ugeni mzito

Dkt. Edwin Paul Mhede

Naibu Katibu Mkuu

Dkt. Edwin Paul Mhede naibu katibu mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi amefanya ziara ya kikazi katika mji wa caserta nchini Italy, ambako ametembelea wadau wenye nia ya uwekezaji katika sekta hiyo. Katika ziara hiyo iliyoandalia kwa kushirikiana na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania mkoani Campania Ms. Judith Joseph akiambatana na Makamu mwenyekiti ndugu Hussein Msawira na katibu wa jumuiya Ms. Cecilia Lemmah. Naibu katibu mkuu alitembelea na kujionea ufugaji wa ng’ombe wa nyama , maziwa pamoja na taratibu,malisho na uchinjaji kwa ujumla.

Naibu katibu mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi pia alitembelea vitendea kazi vya kisasa akiwemo matrekta na zana zingine za kilimo na mifugo.

Ziara hii ilihusu kuja kukutana na wawekezaji ambao tayari walishatembelea Tanzania, lakini ujumbe huo ulifika kujionea uhalisia zaidi wa utendaji kazi kwenye ufugaji wa ng’ombe mpaka bidhaa ya mwisho ya mifugo, lakini jipya zaidi Naibu katibu mkuu pia alikuja kuona jinsi gani Nyati nchini italy anavyotumika kwa ajili ya maziwa na utengenezaji wa Mozzorella cheese. Nyati ambao nchini Tanzania ni wengi na ni wanyama wa porini.

Katika ziara hiyo maalumu Dkt. Mhede aliongozana na mwenyeji wake Mwambata wa kilimo Ubalozi wa Tanzania nchini Italy Madame Jacqueline Boniface Mbuya. (Agricultural Attaché. Alternate Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the UN Rome)

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %