
Balozi Kombo aendelea na nafasi ya Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 17/11/2025 akiwa ikulu ya Chamwino Dodoma , alikutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza baraza jipya la mawaziri. Uteuzi huu wa baraza jipya la mawaziri umefuatia baada ya Uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29/10/2025 ambapo Dr Samia Suluhu Hassan alishinda kwa kishindo na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya sita kipindi cha pili. Rais ameunda baraza la mawaziri lenye wizara 27 , pamoja nao pia ameteu manaibu waziri. Rais pia ameunda wizara mpya ya Vijana Wateule wote wataapishwa siku ya tarehe 18/11/2025.
Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki ni moja ya wizara muhimu katika taifa,Rais amemteua tena Mh. Balozi Mahmoud Thabit Kombo Kuendelea na nafasi ya waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki. Pamoja nae atakuwa na manaibu waziri wawili, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe na Mhe. James Kinyasi Millya.












