
Dar Es Salaam
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, leo Alkhamisi tarehe 4 Disemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) waliopo nchini Tanzania wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU)aliyepo nchini Tanzania, Mhe. Christine Grau walipomtembelea katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Mabalozi hao waliwasilisha taarifa zao pamoja na kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Mazungumzo hayo pia yalijumuisha na kuimarisha diplomasia ya kibunge (Parliamentary Diplomacy) kati ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la Ulaya baada ya kutoa Matamko mbali mbali.
Kikao hicho kimehudhuria na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Balozi wa Finland, Hispania, Italia, Ubelgiji na Ujerumani.















