0 0
Read Time:1 Minute, 8 Second

Diplomasia ya uchumi


Na Kagutta NM | 13/05/2026 Roma

Wadau wa ITALIA-AFRICA Cooperazione Internazionale (wakiongozwa na Rais wa taasisi, Wakili Angela Felicia Senese), Avvenire srl, Marco Polo srl, na COINS Social Enterprise, wamekutana kwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk kwenye kikao cha kwanza mbapo walijadili kwa mapana dhamira yao kuu ya miradi katika sekta ya elimu, wakianzia na lugha na ujuzi mbalimbali ambao utafungua fursa za ajira kwa vijana nje na ndani ya nchi.

Katika mradi wa elimu, Mhe. Balozi aliwataka wadau hao kuangalia pia vijana ambao tayari wana ujuzi nchini Tanzania kupata nafasi za ajira katika taaluma zao ambazo zitahitajika. Pamoja na miradi ya uwekezaji, wadau wamemhakikishia Mhe. Balozi kuwa kuna uwezekano wa kuandaa kongamano la biashara itakapohitajika.

Pia walijadili kuhusu suala la masoko.wadau wamedhamiria pia kusaidia kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo, ambapo Mh.Balozi Mbarouk aliwataka pia kusaidia bidhaa za kilimo kufikia kiwango kinachotakiwa cha Ulaya na kuweza kupata soko la bidhaa hizo nchini Italy; kwa kufanya hivyo itafungua masoko mengine barani Ulaya..”alisisitiza Mh Balozi” Mwisho, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliwahakikishia wadau kuwa katika kutekeleza sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi upo tayari kupokea mpango kazi na kusaidia mchakato mzima kufuatana na taratibu na Sheria za nchi kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa na hatimae kuchangia maendeleo ya nchi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %