1 0
Read Time:1 Minute, 46 Second

Waziri Kombo atuma salamu za rambirambi kwa Watanzania

Na Kagutta NM.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk ameongoza Watanzania nchini Italy kwenye msiba wa Mtanzania Marehemu Mark Mgaya Mdachi aliefariki tarehe 28/08/2026 wakati akipatiwa matibabu hospitalini jijini Rome.

Marehemu alitegemewa kuzikwa leo katika makaburi ya Prima Porta ya jijini Rome lakini kutokana na kukosekana kwa barua ya familia yake ambayo ilitoa ridhaa kwa Balozi na kuridhia kuwa mpendwa wao azikwe Rome badala ya kusafirishwa mwili nyumbani Tanzania, kwa sheria mpya pia inahitaji barua kama hiyo kutoka kwa familia ipelekwe kwenye mamlaka za makaburi ili waweze kutoa kibali cha kuzika.

Hata hivyo kutokana Watanzania walikwisha fika kwa ajili ya mazishi na ukizingati wengine wametokea mikoani, Balozi aliamua zoezi liendelea la sala na maombi na kutoa nafasi kwa watu waliohudhuria kutoa heshima zao za mwisho hasa kwa wale wanaotoka mbali na inawezekana kuwiwa vigumu kusafiri tena siku ya tarehe 1/10/2026 ambayo imepangwa kwa ajili ya kuzika.

Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk ambae ndie mlezi wa Diaspora nchini Italia amewashukuru sana Watanzania waliofika lakini pia kwa wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuchangia msiba wa Mtanzania mwenzao. Balozi aliendelea kusisitiza umoja , mshikamano na upendo kwa Watanzania na kuweka msisitizo wa mawaidha yaliyotolewa na Padre Mashishanga alieongoza misa ya marehemu. Padre Mashishanga wakati akiongoza misa ya marehemu alisisitiza umoja na upendo kwa Watanzania. Padre Renatus Mashishanga ni padre wa Jimbo kuu Katoliki la Tabora Tanzania na kwa wakati huu yupo chuoni Vatican.

Wakati akifunga hotuba yake fupi, Balozi Mbarouk aliwasilisha salamu maalumu za Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo ambaye pamoja na salamu za rambirambi pia alichangia msiba huo. Balozi Kombo kabla ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan, alikuwa balozi nchini Italy ambako ameacha alama ya upendo kwa Watanzania, na sasa Balozi Mbarouk anapita njia zilezile kwani pamoja na majukumu yake mengi lakini bado anashirikiana na Watanzania katika kila jambo la kijamii pamoja na kutatua changamoto zao.

Baadhi ya Watanzania wanaoishi mkoa wa Campania
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %