Na AbuLuLu FaJM
Prince philipo (Philip), Duke wa Edinburgh
Jumba la Buckingham limetangaza kwamba Mfalme Philipo mume wa Malkia Lizabeti amefariki dunia, Asubuhi ya leo, tarehe 9 April 2021.
Habari za kufariki kwa mume wa Malkia Lizabeti, walio oana mwaka 1947, na kujaaliwa watoto wanne, ambao ni; Prince Charles, Princess Anne, Prince Andrew na Prince Edward, zimetolewa muda si mrefu baada ya kufariki kwake.
Habari za kufariki kwake, zimetangazwa kutoka kwenye hekalu la kifalme, jijini London kuwa, Prince Philipo, Amefariki, akiwa na umri wa miaka 99.
Taarifa kutoka Ikulu ya Buckingham ilisema: “Ni kwa huzuni kubwa kwamba Mume wa Malkia wa Uingereza Amefariki Akiwa nyumbani kwake, kwenye kasri ya Buckingham.”
“Mfalme amekufa kwa amani asubuhi ya leo katika Jumba la Windsor.”
Duke Philipo alikuwa ameowana na Malkia Elizabeti wa II kwa zaidi ya miaka 70.









