
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Jumuiya ya Watanzania wanaoishi mkoa wa Campania ITALY wamefanya uchaguzi wa kihistoria Jana jumamosi tarehe 4/06/2022.
Uchaguzi huo ambao uliikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa ulifanyika kwenye Ukumbi wa Hotel La Pace mjini Napoli na ukamalizika kwa Salama na Amani.
Kampeni kubwa ilikuwa ni kwenye nafasi ya Mwenyekiti ambayo ilikuwa ina wagombea wawili, Ndugu Livinus Mwereke na Dada Judith Joseph. Nafasi zingine zilikuwa ni ya Makamu Mwenyekiti, katibu na mweka Hazina.
Ndugu Judith Joseph aliibuka mshindi na kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu ilipoundwa Jumuiya mwaka 2007.
Nafasi zingine kwa kuwa wagombea hawakuwa na wapinzani, kamati ya kusimamia uchaguzi ilipendekeza kwa wapiga kura kuwa wamepita bila kupingwa na Watanzania waliunga mkono kwa makofi mengi na shangwe ya kuwapongeza.
Nae Ndugu Livinus Mwereke baada ya matokeo alipata nafasi ya kutia shukran zake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya na alitumia nafasi hiyo kumpongeza mwenyekiti mpya.
Mwisho mwenyekiti wa Jumuiya Ndugu Judith Joseph aliwashukuru Watanzania kwa kumuamini na kumchagua kwa kura nyingi, hivyo alisema ana deni kubwa kwao na kuwaahidi kuwa hata waangusha. Vilevile ameomba ushirikiano na Wanajumuiya wote Pamoja na viongozi waliopita.
Mchakato mzima wa uchaguzi ulisimamiwa kwa karibu na Mwenyekiti wa kamati ya Diaspora Italy Ndugu Kagutta N. Maulidi,ambaye aliwashukuru Sana wote walioshiriki na kuhakikisha mchakato mzima unafanikiwa kama alivyo elekeza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
Tarehe ya Utambulisho maalumu kwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo ambae ndie mlezi wa Diaspora nchini Italy Pamoja na nchi anazowakilisha,itapangwa alisema mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora.


MATOKEO YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NAPOLI IN CAMPANIA
Mwenyekiti:. JUDITH JOSEPH
Makamu Mwenyekiti: HUSSEIN MSAWIRAJIWE
Katibu: CECILIA REMMY LEMMAH
Hazina: JOSEPHINE LELLO CHUWA








